Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh9 bilioni zatengwa mafunzo ya vijana kujiajiri

New Content Item (1)

Baadhi ya vijana waliopata ufadhiri wa ofisi ya Waziri Mkuu kwenye fani ya uanagenzi katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must) wakimsikiliza Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Joyce Ndalichako leo Jumatano, Agosti 23, 2023. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya kunufaisha vijana katika mafunzo ya uanagenzi ili waweze kujiajiri.

Mbeya. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya kunufaisha vijana katika mafunzo ya uanagenzi ili waweze kujiajiri.

Ndalichako ameyasema hayo leo Jumatano Agosti 23, 2023 baada kufanya ziara  Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na kukagua miundombinu ya elimu ya nadhalia na vitendo kwa vijana waliopata fursa  ya masomo  kupitia  ufadhili wa ofisi ya Waziri Mkuu.

 “Serikali iko kazini msikubali kutumika kama sehemu ya kuvunja amani ya mkatumike kuleta tija za kiuchumi kupitia fursa elimu wanayopata kwa ufadhili wa Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan  ”amesema.

Amesema katika kipindi cha awamu tano za mafunzo ya uanagenzi zaidi ya vijana 133,443 wamenufaika nchini kwenye vyuo mbalimbali na kwamba katika awamu ya sita inayotarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu Serikali imetenga zaidi ya Sh 9 bilioni kwa ajili ya elimu bure kwa vijana 4,500.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amesema fursa hii kwa vijana inapaswa kuchangamkiwa kwani inawajengea wigo mpana wa kwenda kujiajirii na kuajiri wengine.

“Waziri tunashukuru sana kwa fursa hii na nyingine zinazokuja kwa vijana wa kitanzania ,hivyo niwaase kuwa kiumbele kushirikiana na Serikali na kuwapuuza wanasemea vibaya mambo mazuri ya fursa zinazoelekezwa na Serikali kwa maslai mapana kwa taifa ”amesema.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo MUST, Godliving Mtui amesema wanaishukuru Serikali kwa kukiamini chuo hicho na kutoa fedha kwa ajili ya kuendeleza fani 14 kwa vijana wa mafunzo ya uanagenzi.