Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh950 milioni zatengwa kuboresha miundombinu

Muktasari:

  • Serikali imesema Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) imetenga Sh950 milioni za kuboresha miundombinu ya mitaa ya viwanda.


Dodoma. Serikali imesema Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) imetenga Sh950 milioni za kuboresha miundombinu ya mitaa ya viwanda.

Akijibu swali leo Alhamisi Aprili 28, 2022 la Mbunge wa Nyasa (CCM), aliyehoji ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa kituo cha Sido wilayani Nyasa, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema katika bajeti ya mwaka 2022/23 wizara hiyo kupitia Sido imetenga Sh950 milioni za kuboresha miundombinu ya mitaa ya viwanda.

Amesema kati ya fedha hizo, Sh100 milioni ni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha mafunzo na uzalishaji cha Sido wilayani humo.

 “Hivyo, pindi fedha hizo zitakapopokelewa, ujenzi wa kituo hicho utakamilika,”amesema.