Shule za Baobab zaendelea kung’ara kitaaluma

Shule za Baobab zaendelea kung’ara kitaaluma

Muktasari:

Shule za Baobab zipo katika kijiji cha Mapinga, Kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani. Shule hizi zinamilikiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya “Shajar Schools Association”.

Shule za Baobab zipo katika kijiji cha Mapinga, Kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani. Shule hizi zinamilikiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya “Shajar Schools Association”.

Asasi hii iliundwa mwaka 2004 kwa lengo la kuanzisha taasisi za elimu ili kusaidiana na Serikali kupambana na adui ujinga. Mwaka 2005, Shajar Schools Association ilianzisha shule ya Sekondari Baobab na kupewa namba ya usajili S. 1597 ikiwa na jumla ya wanafunzi 70 wote wakiwa wasichana.

Baadaye mkondo wa wavulana ulianzishwa ambao upo umbali wa mita 800 kutoka eneo ulipo mkondo wa wasichana.

Kila mkondo una miundombinu inayojitosheleza kama vile mabweni ya kisasa, maktaba (ikiwemo ya kielektroniki ambapo wanafunzi husoma vitabu wakiwa mtandaoni kwa utaratibu maalum), maabara za kisasa (za sayansi na tarakilishi), ukumbi wa mihadhara, kumbi za mitihani, vyombo vya usafiri, mazingira mazuri na tulivu kwa ajili ya wanafunzi kujifunza. Kwa sasa kuna shule ya awali na msingi Baobab.

Sera ya udahili wa wanafunzi

Shule zinafuata sera ya kudahili wanafunzi wenye uwezo wa wastani, wanaofundishika, wenye ari na nia ya kujifunza. Mwanafunzi anapaswa kupata alama isiyopungua asilimia 50 katika kila somo kwenye mtihani wa usaili ili aweze kujiunga na masomo shuleni Baobab. Kwa kidato cha tano, udahili unazingatia ufaulu wa mwanafunzi kwenye mtihani wa Taifa wa kidato cha nne.

Ili mwanafunzi ajiunge na masomo hayo, anapaswa kuwa na ufaulu wa daraja la kwanza au la pili na “credit” tatu katika masomo ya tahasusi (Combination) anayoiomba.

Mtaala

Shule za Baobab zinafundisha kwa kufuata mtaala wa Tanzania. Walimu hufundisha kwa ubora wa hali ya juu ambapo mikakati thabiti huwekwa ili kuendeleza uwezo, akili, vipaji, udadisi na ubunifu wa wanafunzi. Kwa Sekondari, elimu inayotolewa inaanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.

Masomo yanayofundishwa kwa kidato cha kwanza hadi cha nne: Hisabati, Historia, Jiografia, Uraia, Fizikia, Kemia, Baolojia, Uhasibu, Biashara, Kompyuta, Kiswahili, Kiingereza, Fasihi, Kiarabu, Kichina, Biblia na Elimu ya Dini ya Kiis-lam. Kwa kidato cha tano na sita kuna michepuo ya sayansi (PCM, PCB, PGM, CBG), biashara (ECA, HGE na EGM) na sanaa (HKL, HGK, HGL).

Taaluma

Shule za Baobab zimekuwa zikifanya vizuri katika mitihani ya ndani na ya Taifa. Mwaka 2020, jumla ya wanafunzi 32 walifanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne. Kati yao, wanafunzi 22 walipata wastani wa alama “A”, 5 alama “B” na 5 walipata alama “C”. Kwa Shule ya sekondari, mwaka 2014, ilitoa mwanafunzi bora namba 01 Tanzania (Tanzania One) katika mitihani ya kidato cha 4. Mwaka huo pia ilitoa mwanafunzi bora namba 06 kwa masomo ya biashara kwenye matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita.

Aidha, mwaka 2015 shule ilitoa mwanafunzi bora namba saba kwa watahiniwa wa kike katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne. Zaidi ya hayo, mwaka 2019, shule ilitoa mwanafunzi bora namba moja Tanzania (Tanzania One) kwa masomo ya biashara katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita.

Mwaka 2020, shule ilitoa mwanafunzi bora namba nne kwa masomo ya biashara katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha 6. Katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2020, jumla ya wanafunzi 113 walipata daraja la kwanza, 74 la pili, 26 la tatu na 03 walipata daraja la nne. Kwa Kidato cha pili, jumla ya wanafunzi 221 walipata daraja la kwanza, 46 la pili, 10 la tatu na 03 la nne. Hakuna mwanafunzi aliyefeli katika mitihani hiyo ya Taifa.

Siri ya kufanya vizuri kitaaluma

• Walimu wenye sifa stahiki, wenye uzoefu na wanaojituma katika kufundisha

• Mikakati imara ya kuinua ufaulu wa wanafunzi.

• Miundombinu bora na wezeshi kwa wanafunzi kujifunza.

• Mazingira bora na tulivu kwa wanafunzi kujifunza

• Uongozi imara wa shule ambao unawajali wafanyakazi kwa kuwapatia motisha mbalimbali na hivyo kuinua ari na moyo wa kujituma kazini kwa utulivu.

• Maadili bora ya mtoto wa kitanzania. Wanafunzi wanalelewa kwenye maadili mazuri na kila mmoja ana uhuru wa kuabudu kulingana na imani yake.

• Uwepo wa zahanati ndani ya eneo la shule inayorahisisha matibabu kwa wakati.

• Chakula bora ambacho ni mlo kamili (balanced diet) hutolewa kwa wanafunzi ili kuimarisha afya ya mwili na akili. • Wanafunzi wote hushiriki katika michezo mbalimbali ili kuimarisha afya zao.

Hitimisho

Mtoto anaposoma shule za Baobab anakuwa katika mikono salama. Wanafunzi hupewa malezi bora yanayozingatia utamaduni wa Mtanzania. Aidha, mwanafunzi wa Baobab ana nafasi nzuri ya kufaulu mitihani na hivyo kutimiza ndoto zake kwa kupata elimu bora.

Shule za Baobab zimekuwa zikiandaa wataalam wengi na viongozi kwenye nafasi mbalimbali kama vile Udaktari, Uhasibu, Uhandisi, Ubunge, Ukuu wa Wilaya, na Uhadhiri katika Vyuo Vikuu. Ni vema ukamtafutia mwanao shule bora inayokwenda na wakati ili apate elimu bora itakayomuwezesha kujikwamua kiuchumi, kinidhamu, kiakili na kimaadili.