Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sita kortini wakidaiwa kuiba kilo 54 za mawe ya dhahabu

Muktasari:

Watu sita wakazi wa Wilaya ya Geita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita wakikabiliwa na shtaka la wizi wa kilo 54.1 za mawe yanayosadikiwa kuwa na dhahabu.

Geita. Watu sita wakazi wa Wilaya ya Geita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita wakikabiliwa na shtaka la wizi wa kilo 54.1 za mawe yanayosadikiwa kuwa na dhahabu.

Washtakiwa hao Musa Ramadhan (27), Richard Bora (33), Patrick Kwezi (26) Masood Salim (32), Revocuts Elaxanda (36) na Erick Daniel (28) wanadaiwa kufanya kosa la wizi kinyume na kifungu cha 258 (1) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu.

Mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi Johari Kijuwile, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Kabula Benjamen ameeleza Mahakma kuwa Julai 23, 2023 washtakiwa hao kwa pamoja saa 3:30 usiku huko katika mgodi wa GGML katika eneo la Loncon pit bila kuwa na kibali waliiba mawe kilo 54.1 yanayodhaniwa kuwa na dhahabu.

Amedai mahakamani hapo kuwa mawe hayo yanadhaniwa kuwa na dhahabu gramu 0.53 yenye thamani ya zaidi ya Sh150,000 ambayo ni mali ya mgodi wa dhahabu wa Geita(GGML).

Washtakiwa hao wamekana kutenda kosa hilo huku, upande wa mashtaka ukidai upelelezi haujakamilika na kesi kuahirishwa hadi Septemba 4, 2023 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa hao wako nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti yakuwa na mdhamini mmoja atakayesaini hati ya Sh 300,000 pamoja na barua ya utambulisho kutoka kwenye eneo wanakotoka.