Sita wadakwa mkoani Mbeya wakihusishwa na mtandao wa uhalifu

Muktasari:

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewakamata watu sita kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa uhalifu, wakidaiwa kuvunja nyumba kuiba vifaa mbalimbali pamoja na kuiba pikipiki.

Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewakamata watu sita kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa uhalifu, wakidaiwa kuvunja nyumba kuiba vifaa mbalimbali pamoja na kuiba pikipiki.

Amesema watu hao wanafanya matukio hayo maeneo ya mkoa huo na mikoa jirani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei ameeleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari  leo Ijumaa Novemba 27,2020 akisisitiza kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia silaha mbalimbali kufanikisha uhalifu huo.

"Tulipopata taarifa tulianza msako na kufanikiwa kuwatia nguvuni na walipohojiwa wamekiri kuhusika na matukio ya uhalifu na kuonyesha maeneo walikohifadhi silaha.”

"Walipofanya upekuzi walikamata  pikipiki za matairi matatu, pikipiki mbili, majiko ya gesi, magodoro, televisheni, redio nne, baiskeli na vitu vingine mbalimbali vya majumbani,” amesema.

 Matei amesema kuwa kipindi cha mwisho wa mwaka kumekuwa na matukio mengi ya uhalifu na kuomba watendaji, madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa kulisaidia jeshi la polisi kudhibiti.