Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siyo GIFs pekee, sasa utaweza kuweka komenti kwa picha Instagram

Muktasari:

  • Sasa unaweza kujibu ‘comment’ kwa kuweka picha kwanza unatakiwa kusasisha (update) Instagram yako.

Dar es Salaam. Mtandao wa kijamii wa Instagram umekuja na kipengele kipya kinachoruhusu watumiaji wake kuweka picha (photo) moja kwa moja kwenye sehemu ya maoni (comments), hatua inayotajwa kuongeza msisimko kwa watumiaji.

Kipengele hicho kipya kinawapa watumiaji uwezo wa kutoa maoni kwa kutumia picha pamoja na maandishi, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo maoni yalitolewa kwa maandishi, emoji (☺️) au GIF pekee.

Mabadiliko hayo mapya yameanza kuonekana kwa awamu kuanzia Mei na Juni, 2026, ambapo watumiaji kadhaa nchini na duniani kote wameanza kushuhudia alama ya kamera (camera icon) ikionekana pembeni mwa kisanduku cha kuandikia maoni.

Instagram inasema maboresho haya yanalenga kuwasaidia watumiaji kueleza hisia zao kwa upana zaidi bila kulazimika kutumia maandishi pekee au picha fupi za vionjo (GIFs) kama ilivyokuwa awali.

Hata hivyo, kipengele hicho bado hakijafikiwa na watumiaji wote kwa wakati mmoja kutokana na utaratibu wa kiteknolojia unaojulikana kama ‘staged rollout’ usambazaji wa awamu.

Hata hivyo, maoni ya picha ni utaratibu wa kawaida katika mitandao mingine ya kijamii kama Facebook na X zamani Twitter.

Mabadiliko hayo yanakuja wakati Instagram ikiendelea kuongeza vipengele vipya ili kushindana na majukwaa mengine ya mitandao ya kijamii.

Katika miezi ya hivi karibuni, kampuni hiyo imezindua huduma ya “Instants” inayoruhusu watumiaji kutuma picha zinazopotea baada ya kutazamwa.

Bila kusahau uwezo wa kuhariri maoni (edit), yaliyokwisha kuchapishwa ndani ya dakika 15 tangu yawekwe.