Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SNV: Limeni mazao himilivu

Mshauri mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV), Godfrey Kabuka akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wakulima, wasindikaji na wataalamu wengine wa Kilimo SNV ilipowakutanisha kwa lengo la kujadili athari za mabadiliko hayo na kilimo cha alzeti. Lilian Lucas

Muktasari:

  • Wakulima nchini wameshauriwa kulima mazao yanayostahimili mabadiliko ya tabia ya nchi likiwemo zao la Alizeti ambalo wataalamu wanasema likilimwa kwa kuzingatia utaalamu na kanuni za kilimo litaongeza tija kwa wakulima.

Morogoro. Wakulima nchini wameshauriwa kulima mazao yanayostahimili mabadiliko ya tabia ya nchi likiwemo zao la alizeti ambalo wataalamu wanasema likilimwa kwa kuzingatia utaalamu na kanuni za kilimo litaongeza tija kwa wakulima.

Aidha kutokana na mabadiliko hayo ya tabia ya nchi kuanza kuathiri baadhi ya maeneo, wadau wa kilimo wamekuwa wakipata athari za mazao yao.

Mshauri Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) Godfrey Kabuka amesema hayo jana baada ya shirika hilo kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wakulima, wasindikaji na wataalamu wengine kwa lengo la kujadili athari za mabadiliko hayo na kilimo cha Alizeti.

“Wadau hawa wamekuwa wakikukata na athari hizi hivyo kuna haja ya kuwa na namna bora ya kukabiliana na hali hii na hivyo kunusuru sekta ya kilimo iepuke athari zinazoweza kujitokeza,” amesema.

Amesema mwaka 2019 mradi wa Graft kipande cha kilimo ulifanya tathimini ya athari ya mabadiliko ya hali ya hewa na taarifa hiyo ilikuwa haijawafikia wadau wengi hivyo wadau watafahamu kwa namna gani mabadiliko ya tabia nchi yatakuwa kwa miaka mitano, kumi na ishirini ijayo.

“Tathimini hii ilionyesha kwamba maeneo ambayo sasa yanalima Alizeti miaka ijayo yatakuwa hayafai kwa kilimo hicho, kwahiyo tunatakiwa kuwa na timu ya watu wa zao hilo ili kujadili mbinu zinazofaa ambazo kwazo wadau na wakulima wataendelea kulima kwa tija,” amesema.

Mwanasayansi mtafiti wa masuala ya usimamizi wa ardhi na mabadiliko ya tabia nchi na kilimo himilivu Dk John Recha amesema nia ya kushiriki kwenye mradi huo ni kufanya uchunguzi hasa mabadiliko ya tabia nchi na yanavyoendelea nchini na kufanya maeneo mengi kuwa kame na kwamba kilimo himilivu kinaweza kufanyika maeneo tofauti nchini.

Dk Recha amesema zao la Alzeti ndilo linalostahimili mabadiliko ya tabia nchi lakini wakulima wanatakiwa kutumia mbinu zinafaa ili iweze kuzalishwa vyema zaidi na kwamba wakitumia mbegu ambazo sio bora na kuanza kupanda kwa kutozingatia ushauri wanaweza kupata athari.

Katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro Mussa Ali Mussa ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa huo kupanda miti na kuitunza kudhibiti mabadiliko hayo hususani miti ya karafuu ili iwasaidie pia kwa kipato.