Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Songwe waomba miundombinu ya umwagiliaji

Muktasari:

Baadhi ya wakulima wanaojihusisha na kilimo cha umwagiliaji, wameiomba Serikali kuwatengenezea miundombinu ya umwagiliaji Ili waweze kuimarisha shughuli zao huku wakiendelea kuhifadhi vyanzo vya maji.

Songwe. Baadhi ya wakulima wanaojihusisha na kilimo cha umwagiliaji, wameiomba Serikali kuwatengenezea miundombinu ya umwagiliaji Ili waweze kuimarisha shughuli zao huku wakiendelea kuhifadhi vyanzo vya maji.

 Wakizungumza leo Jumatano Oktoba 19, mwaka huu kwa nyakati tofauti wakulima kutoka Ihanda wamesema wamekuwa wakifanya kilimo hicho kwa hofu kutokana na kuwa kinyume cha sheria ya mazingira inayokataza kufanya shughuli za kilimo ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji.

Mmoja wa wakulima hao Maison Mwamlima amesema wanashindwa kufanya shughuli zao nje ya mita 60 kwa sababu ya kukosa miundombinu rafiki kuwezesha walime kwa ufanisi na tija.

"Tunatumia maji yanayotiririka Ili kujiajiri kwenye uzalishaji wa mazao ya mbogamboga katika kipindi cha kuangazia Ili kujipatia kipato," amesema.

Naye James Mulungu kutoka Mbimba amesema Mamlaka ya Bonde la Ziwa Rukwa imeanza kuwatoza vibali vya kutumia maji hayo na kufanya washindwe kumudu na kukiona kilimo hicho kuwa kigumu.

"Tumeanza kutakiwa kulipia vibali bila kutolewa elimu ya ili tupate uelewa wa kutosha," amesema Mulungu.

Mwenyekiti wa maji Bonde la Ziwa Rukwa na Mto mdogo wa Mlowo, Paul Magesa  amekiri kupokea malalamiko ya watumia maji kwenye vyanzo vya maji wakidai hawana elimu kuhusu ya vyanzo vya maji si za kweli bali elimu imetolewa katika maeneo mbalimbali na kuwa hata hivyo itaendelea kutolewa.

Magesa amefafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria za maji haitakiwi kufanya shughuli za kilimo ndani ya mita 60 kwenye chanzo cha maji na ikibainika ni hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yake.

"Kilimo cha umwagiliaji wa kutumia mashine lazima mkulima aombe kibali kwa Sh250, 000 na endapo akikubaliwa anaweza kutumia mitambo yake kwa ajili ya umwagiliaji," amesema Magesa.

Amesema vyanzo vya maji vinatakiwa kutunzwa ili kulinda mazingira yetu kwani kila mwananchi anajukumu la kuvilinda.