Spika asubiri uamuzi wa mahakama wabunge 19 waliofukuzwa Chadema

Hatima ya Halima Mdee, wenzake 18 kuamuliwa mahakamani

Muktasari:

  • Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema anasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema anasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Dk Tulia Akson amesema wabunge hao wataendelea na ubunge mpaka pale uamuzi wa mahakama utakapotolewa.

Dk Tulia amesema hayo leo Jumatatu Mei 16, 2022 wakati akitoa maelezo kuhusu wabunge hao ambao walivuliwa uanachama na Chadema.

Katika maelezo yake, Dk Tulia amesema kuwa amepata taarifa kutoka kwa wabunge hao kuwa tayari wameshafungua kesi  Mahakama Kuu ya kupinga mwenendo wa kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu na baadaye Baraza Kuu kukataa rufaa yao.

“Bunge haliwezi kuingilia mchakato huo mpaka Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi, ninalazimika kutokutangaza kuwa nafasi za viti maalumu 19 vya Chadema viko wazi mpaka pale mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi” amesema Dk Tulia

Spika amekiri kupokea barua za pande mbili ikiwemo ya Chadema ambao walimtaarifu kuhusu kuwafukuza uanachama wabunge hao 19 wa Viti Maalum.

Nyingine ni barua ya wabunge hao ambayo inaeleza kuwa wamefungua kesi mahakamani kupinga kitendo hicho kwa madai ya kufukuzwa kwao hakukuwa na msingi na kuna vitu havikuwa sawa.

“Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, chombo pekee chenye kutoa haki ni mahakama na hivyo kwa kuwa hawa wamekwenda mahakamani kupinga kufukuzwa kwao, jambo hili linatakiwa kuachwa kwanza hadi hapo mahakama itakaposema vinginevyo,” amesema Dk Tulia.

Huku wabunge wakiwa wanapiga makofi kwa nguvu kutoka pande zote, Spika alitangaza kuwa kuanzia leo anafunga mjadala wa kuzungumzia jambo la wabunge hao kutoka kwa mtu yeyote na kwamba kama kuna mtu anataka kujua kuhusu ubunge wao msemaji pekee atakuwa ni yeye Spika.

Wakati Spika akitoa kauli hiyo, kati ya wabunge 19 wanaotajwa, walikwepo 10 ambao baadhi yao mapema walishapewa maswali ya kuuliza mmoja akiuliza swali la msingi lakini watatu waliuliza maswali ya nyongeza.

Alhamisi iliyopita kikao cha juu cha maamuzi kuhusu masuala ya kinidhamu kutupilia mbali rufaa ya wabunge hao kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama Novemba 27, 2020.

Kikao hicho cha Baraza Kuu la Chadema kilichofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, wajumbe walipopiga kura nyingi za kubariki kufukuzwa kwao.

Hata hivyo, baada ya uamuzi huo, licha ya kutarajiwa na wanachama wengi wa Chadema, haukutarajiwa na wabunge hao na Halima Mdee, kiongozi wa wabunge hao na aliyekuwa mwenyekiti wa Bawacha alisema:

“Kilichofanyika pale ni uhuni wa kiwango cha hatari. Hata Mbowe mwenyewe anajua.