Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sukari ya magendo yagawanywa kwa wahitaji mkoani Songwe

Muktasari:

Zaidi ya kilo 4,880 za sukari yenye thamani ya zaidi ya Sh13.2milioni zilizokuwa zinaingizwa nchini kwa magendo na kukamatwa, zimegawanywa kwenye taasisi mbalimbali Mkoani Songwe leo Januari 5. 

Songwe. Zaidi ya kilo 4,880 za sukari yenye thamani ya zaidi ya Sh13.2milioni zilizokuwa zinaingizwa nchini kwa magendo na kukamatwa, zimegawanywa kwenye taasisi mbalimbali Mkoani Songwe leo Januari 5. 
Mkuu wa Mkoa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela amegawa sukari hiyo kwa taasisi za Magereza, Hospitali, shule na kwenye kituo cha kulelea watoto yatima.
Akizungumza wakati wa ugawaji huo, Brigedia Jenerali Mwangela amewaonya wafanyabiashara kuacha kuingiza sukari nchini kwa magendo kwani kufanya hivyo kunaweza kuwasababiahia kufilisika watakapokamatwa. 
Naye Mkuu wa wilaya ya Momba Mkoani hapa Jumaa Said Irando amesema wamefanya operesheni kukamati Mali za magendo ambazo haziruhusiwi kuingizwa inchini ikiwemo sukari.