Suma JKT kujenga bandari kavu Ruvu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Muktasari:
- Ujenzi huo utakaogharimu Sh7 bilioni utapunguza idadi kubwa ya mizigo bandarini na kurahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam kwenda sehemu mbalimbali nchini.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) imetiliana saini mkataba na kampuni ya Suma JKT kuanza ujenzi wa bandari kavu (ICD) Ruvu mkoani Pwani itakayokuwa na ukubwa wa hekta 500.
Ujenzi huo utakaogharimu Sh7 bilioni utapunguza idadi kubwa ya mizigo bandarini na kurahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam kwenda sehemu mbalimbali nchini.
Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko na Mshauri Mkuu wa Mambo ya Kisheria wa Suma JKT, Kanali John Mbungo mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.