Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taasisi ya kichina UDSM yazindua kitabu cha kujifunza kichina kilivyotafsiriwa kwa Kiswahili

Muktasari:

  • Tayari UDSM ipo katika mpango wa kuanzisha shahada itakayojikita katika masomo ya kichina na Kiswahili kwa lengo la kuongeza wigo na fursa ya soko la ajira.

Dar es Salaam.Taasisi ya kufundisha lugha ya kichina ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),imezindua kitabu cha kujifunza lugha ya kichina iliyo na tafsiri ya lugha ya Kiswahili.

Kitabu hicho ambacho kimepewa jina la ‘Mtazamo wa jumla kuhusu China’ kitawanufaisha wanafunzi watakaojifunza lugha ya kichina wakiwemo wanaosomea stahahada na shahada ya lugha ya kichina na wale wanaosomea ngazi ya cheti na kozi fupi katika lugha hiyo.

Hatua hii inakuja ikiwa tayari chuo hicho kilishatangaza mpango wake wa kuelekea kuanzisha shahada itakayojikita katika masomo ya kichina na Kiswahili kwa lengo la kuongeza wigo na fursa ya soko la ajira

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo upande wa China, Profesa Zhang Xiaozhen,, amesema Rais wa China, Xi Jinping , amekuwa akisisitiza umuhimu wa kujengwa ushirikiano  wa kiutamaduni na hatimaye kuifanya jamii kuishi kwa ushirikino na kuifanya dunia kuwa sehemu  salama na rafiki.

“Hivyo kupitia kitabu hiki ni mwendelezo wa kutimiza maono hayo ya Rais wetu ambapo wajifunzaji wa  lugha ya kichina sio  tu  kitawafanya kujifunza lugha ya kichina bali kupata taarifa mbalimbali  ikiwa ni pamoja na shughuli za kiutamaduni kuhusu nchi ya China.

Profesa Zhang amesema katika uandishi wa kitabu hicho, mambo yaliyozingatiwa ni pamoja na ukweli ili kuhakikisha mwanafunzi anakuwa na uelewa mzuri katika ujifunzaji wake  na kuepuka kukutana na changamoto zisizo za lazima.

“Taarifa zilizopo ndani ya kitabu hicho   zimetoka katika vyanzo vya kuaminika na pia vimewekwa mazoezi mbalimbali vitavyowasaidia wasomaji wake,”amesema Mkurugenzi huyo.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Kichina upande wa Tanzania, Dk Hans Mussa, amesema kitabu hicho kitawanufaisha wanafunzi watakaojifunza lugha ya kichina wakiwemo wanaosomea stahahada na shahada ya lugha ya kichina, wanaosomea ngazi ya cheti na kozi fupi.

Dk Musa amesema kitabu hicho kina sura 12 na mada 19 zinazolenga maeneo mbalimbali ikiwemo kuhusu China , lugha na maandishi ya kichina, Miji mikuu ya Kale ya China, miji  maarufu nchini China.

“Nyingine Dk Mussa amesema ni  Sikukuu za jadi, shughuli za kiutamaduni, vyakula maarufu, fasihi ya kale , mavazi ,tiba za jadi, michezo shughuli za kilimo na miundombinu,”amesema Mkurgenzi huyo.

Aisha amesema kitabu hicho kimeandikwa  kwa ushirikiano wa wakurugenzi wa zamani wa Taasisi ya kichina, walimu wawili wa lugha ya kichina kutoka China na walimu wawili wazawa wa lugha ya kichina wa nchini Tanzania.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Profesa  Bonaventure Rutinwa, amesema uandishi wa kitabu hiki ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Chuo Kikuu yanayohusu utafiti na uchapishaji.

“Hapa ninawapongeza sana Taasisi ya Confucius kwa uamuzi huu wa busara wa kufanya utafiti na hatimaye kuchapisha vitabu hivi.

“Jambo la kutia moyo zaidi ni kuwa uandishi wa kitabu hiki umewahusisha wakurugenzi pamoja na walimu wa Taasisi ya Confucius.

“Aidha, kitabu kimepata heshima ya kuandikiwa dibaji na Balozi wa China nchini Tanzania.Hongereni sana Taasisi ya Confucius kwa kazi hii ya kutiliwa mfano. Ninaamini kwamba huu ni mwanzo, na machapisho mengi zaidi yataandikwa.

“Kwani utafiti na uchapishaji wa vitabu hivi ni njia muhimu ya kuendeleza uhusiano wa kijamii baina ya China na Tanzania,”amesema Profesa  Rutinwa.

Naye Mwenyekiti wa kampuni iliyochapisha kitabu hicho ya Changjiang Publishing & Media Co., Li Zhi, amesema wanashukuru kuaminiwa kuchapa kitabu hicho na kueleza ni mwanzo mzuri wa kuendelea kufanya kazi na taasisi hiyo katika kuchapisha vitabu vingi zaidi huko mbele na hivyo kuimarisha ushirikiano wa kiutamaduni kati ya Tanzania n a China.

Kwa upande wao wanafunzi akiwemo Menasi Ngonyani, amesema wanashukuru kupelekewa kitabu hicho ambacho wanaamini kitawaongeza uwezo wao  wa kujifunza zaidi kichina pamoja na tamaduni zake kwa kuwa ukijua tamaduni pia inakurahisishia ni nini uongee na wapi na wakati gani.

Wakati  Aisha Yahaya, amesema kilichomvutia ni kitabu kuwa na michoro ya maeneo mbalimbali na hivyo kuwarahishia kujua China ikoje hivyo siku wakienda wanakuwa  tayari na picha kichwani.