Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tabibu adaiwa kujiua aacha ujumbe akiwaomba radhi wazazi wake

Mama wa marehemu  Fimbo Ncheye (mwenye nguo za blue)akilia nje ya chumba cha kuhifandhia maiti katika hospitali ya Mji Geita pembeni ni ndugu walioambatana nae kutoka wilaya ya  Sengerema mkoani Mwanza.

Muktasari:

  • Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Thomas Mafuru amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ofisa tabibu huyo alikuwa akijitolea na hakuwahi kueleza  kuwa tatizo.

Geita. Ofisa tabibu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Geita, Fimbo Ncheye anadaiwa kujiua akiwa kwenye chumba alichokuwa amelala, huku akiacha ujumbe wa kuwaomba radhi wazazi wake kwa hatua alizochukua na kutaka mtu yeyote asilaumiwe juu ya kifo hicho.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Thomas Mafuru amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ofisa tabibu huyo alikuwa akijitolea kwenye kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD) na hakuwa mgonjwa na hakuwahi kueleza iwapo ana tatizo lolote.

“Imetokea ghafla, tumepigiwa simu na kuambiwa mwenzetu amefariki kwenye chumba na hii ni kesi ya polisi, naomba nisieleze sababu za kifo. Hadi anaondoka kazini jana, alikuwa vizuri, hakuwa na shida yoyote. Ametibu wagonjwa bila shida, yaani hii imetokea tu ghafla,” amesema.

Ofisa Tabibu Geita adaiwa kujiua, awaachia ujumbe wazazi wake

Dk Mafuru amesema hadi sasa hawajafanya uchunguzi kujua chanzo cha kifo na kwamba wanasubiri taratibu za kipolisi pamoja na familia, ili mwili wake ufanyiwe uchunguzi.

Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa nyumba aliyofia ofisa tabibu huyo, Proses Mwiseo amesema saa tano usiku aligongewa na wapangaji wakidai wanasikia kelele za fujo kama mtu anaugulia na kuomba msaada, lakini walipofika walikuta kelele zimetulia na walipogonga hakufungua mlango.

Marco Madoshi, balozi  wa shina namba tatu katika Mtaa wa Lwenge, amesema baada ya kutoa taarifa polisi walifika na kuvunja mlango na kumkuta kijana huyo yuko kwenye uvungu wa kitanda na ndani ya chumba kulikuwa na dawa zilizopondwa pamoja na dawa ya hospitali pamoja na sindano ambayo haijatumika.

Madoshi amesema hakuna anayejua sababu zilizochangia achukue uamuzi huo na kuwashauri vijana wakiwa na changamoto kuomba ushauri au kusema badala ya kuamua kujiua na kuacha familia ikiwa na majonzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Adam Maro alipotafutwa na Mwananchi Digital amesema yupo kwenye ofisi nyingine na kuomba kupewa muda, ili afuatilie tukio hilo.