Taliban waahidi 'mabadiliko', wananchi wakimbia

Taliban waahidi 'mabadiliko', wananchi wakimbia

Muktasari:

  • Kikundi kilichopindua serikali cha Taliban kimesema kinataka mapatano, kikiahidi kutolipiza kisasi kwa wapinzani na kuahidi kuheshimu haki za wanawake, ikiw ani uongozi tofauti na uliokuwepo Afghanistan miaka 20 iliyopita.


Kabul, Afghanistan (AFP). Kikundi kilichopindua serikali cha Taliban kimesema kinataka mapatano, kikiahidi kutolipiza kisasi kwa wapinzani na kuahidi kuheshimu haki za wanawake, ikiw ani uongozi tofauti na uliokuwepo Afghanistan miaka 20 iliyopita.

Hatua hiyo ilitangazwa Jumanne usiku muda mfupi baada ya kurejea to Afghanistan kwa muasisi wa mwenza, na kuhitimisha kurejea kusikotarajiwa baada ya kuondolewa na majeshi yaliyoongozwa na Marekani mwaka 2001.

Kukiwa na wasiwasi mkubwa duniani kote dhidi ya rekodi mbaya ya haki za binadamu kwa wanamgambo hao wa Taliban -- na maelfu ya watu wakijaribu kuikimbia nchi -- kundi hilo lilifanya mkutano na waandishi wa habari jijini Kabul.

"Wote hao walio upande tofauti wamesamehewa kuanzia A hadi Z," msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid aliwaambia waandishi wa habari wa ndani na nje, akijitambulisha kwa mara ya kwanza.

"Hatutalipiza kisasi."

Mujahid alisema utawala mpya utakuwa "tofauti" kulinganisha na utawala wao wa mwaka 1996-2001, ambao ulijulikana kwa kuua kwa mawe, wasichana kuzuiwa kusoma na wanawake kuzuiwa kufanya kazi na wanaume.

"Kama swali ni kuhusu dini na imani, hakuna tofauti... lakini kama tukichambua kwa kuangalia uzoefu, ukomavu na kwa undani, hakuna shaka kuwa kuna tofauti nyingi," Mujahid aliwaambia waandishi.

Pia alisema "wamepania kuruhusu wanawake kufanya kazi kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislamu", bila kuweka bayana.

Msemaji wa kundi hilo jijini Doha, Suhail Shaheen, alikiambia kituo cha televisheni cha Sky cha Uingereza kuwa wanawake hawatatakiwa kuvaa burga ambayo inafunika karibu mwili mzima, lakini hakusema ni nguo za aina gani zinakubalika.

Hata hivyo, wananchi wa Afghanistan na wageni waliendelea kuitoroka nchi, huku Marekani na mataifa mengine yakiingilia kazi ya kuwaondoa kutoka uwanja wa ndege wa Kabul.

Baadhi ya picha zilizopigwa uwanja wa ndege zinaonyesha maelfu ya watu wakikimbia pembeni ya ndege ya kijeshi ya Marekani wakati ikielekea sehemu ya maegesho.