Tanesco yakata umeme Rufiji kutokana mafuriko

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limekata umeme wilayani Rufiji ikiwa ni siku chache tangu kusambaa video ikionyesha mafuriko yameleta maafa na kuzingira nyumba hadi usawa wa bati.
Video hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha waandishi wa habari wakitumia boti kuzunguka mitaani kuangalia maafa yaliyotokea.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema wamefikia hatua hiyo ili kuepusha maafa kwa wakazi zaidi ya 12,000 wanaoishi kata ya Muhoro waliokubwa na tatizo hilo zaidi.
"Janga hili ni kubwa la mafuriko tumeona kiusalama ni vyema kuondoa huduma ya umeme ili kuepusha maafa kwa wananchi na mali zao," amesema Mgalu.
Mgalu amesema kuwa kwa baadhi ya maeneo ambayo hajafikiwa na mafuriko watarudisha umeme kupitia laini mbadala.
Kadhalika Mgalu alieleza ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utasaidia kudhibiti mafuriko wilayani humo kwasababu bwawa litakuwa linahifadhi maji mengi ili kuzalisha umeme.
"Maji yatakuwa yakiachiwa kwa utaratibu maalum na kuondoa uwezekano wa majanga ya mafuriko kwa miaka ijayo.