Tanzania kutumia umeme wa jua kupitia msaada wa AFD

Muktasari:

  • Katika Wilaya ya Kishapu, Shinyanga, TANESCO inategemea kujenga mtambo mkubwa wa kwanza wa uzalishaji wa umeme wa jua Tanzania (Large scale photo-voltaic-PV).

Katika Wilaya ya Kishapu, Shinyanga, TANESCO inategemea kujenga mtambo mkubwa wa kwanza wa uzalishaji wa umeme wa jua Tanzania (Large scale photo-voltaic-PV).

Utakuwa ni mtambo wa kwanza nchini, lakini siyo wa mwisho. Kwa mujibu wa Wakala wa Nishati wa Kimataifa, barani Afrika, umeme wa kuzalishwa kwa jua unakuwa “mfalme mpya” wa umeme na unatabiriwa utakuwa chanzo cha uzalishaji umeme kinachokua kwa kasi Afrika kufikia mwaka 2040.

Uzalishaji wa umeme unaotegemea jua umeifanya nishati ya umeme kuwa nafuu zaidi duniani huku utendaji kazi ukiimarika maradufu.

Kwa kuongezea, mitambo wa PV unaweza kuongeza Mega Watts (MW) kirahisi hivyo ni rahisi kuufunga na kuutunza. Changamoto za kiuendeshaji na athari zake kwa mazingira na kwa jamii ni ndogo.

Tanzania kutumia umeme wa jua kupitia msaada wa AFD

Chanzo hiki cha nishati bila shaka hakina malipo yoyote, ni jadidifu na hudumu milele. Umeme wa jua pia unachangia uhuru wa kimkakati na ushindani wa nishati wa nchi, kuhamasisha matumizi ya rasilimali za nchi zilizopo na kuepuka utegemezi wa kupanda na kushuka kwa bei ya hydrocarbon.

Zaidi, mitambo ya umeme wa jua ya PV inachochea maendeleo na kupambana na mabadiliko ya tabiachi, ikichangia kidogo katika uharibifu wa mazingira kulinganisha na makaa ya mawe au mitambo ya gesi.

Kwa sababu zote hizi, za kiuchumi, kimkakati na kiikolojia, Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), linashawishika kuwa umeme wa kuzalishwa kwa jua ni mojawapo ya vyanzo vya baadae vya nishati kwa Afrika na hivyo Shirika limeamua kusaidia zaidi kifedha miradi ya umeme wa jua barani Afrika kwa kutoa mikopo nafuu.

Katika wilaya ya Kishapu, Shinyanga, TANESCO itajenga mtambo wa PV wa kwanza wa uzalishaji wa umeme wa jua utakaounganishwa na Gridi ya Taifa na kuwa mtambo wa pili kwa ukubwa wa uzalishaji wa umeme wa jua katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mtambo huu utakuwa na uwezo wa kuzalisha MW 50 na utazalisha kila mwaka 91,600 MWh, wakati huo huo utapunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa 22,400 tCO2 eq. Kwa kuamini kwamba kwa nguvu ya umeme huu wa jua wa Tanzania na kuridhishwa na mafanikio ya mtambo huu wa kwanza wa PV ambao utafungua njia kwa mitambo mingine, iwe ya sekta binafsi au ya umma, AFD imejipanga kutoa jumla ya Euro 130 milioni kufadhili uwekezaji huu na pia ukarabati wa gridi ili kuwezesha nishati ambazo ni nadra kupatikana.

Ni kweli, kumiliki umeme wa jua ni sawa na kumiliki vipindi: wakati wingu linaficha jua, hakuna nguvu inayozalishwa na hakuna umeme unaolisha Gridi ya Taifa. Ili kujenga uwezo katika teknolojia hii mpya, AFD itaisaidia TANESCO kiufundi na kuwasaidia wataalamu wake kufanya ziara maeneo mengine ya umeme wa jua barani Afrika.

Ili kuweza kufanikiwa hivyo, Misaada maalumu itatolewa kwa ajili ya mafunzo, kujenga uwezo na kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Ufaransa, ambayo ujuzi wake katika teknolojia ya masuala ya umeme wa jua unaheshimika.

Mradi huu ni hatua muhimu kwa Tanzania kuelekea katika usambazaji wa nishati safi na endelevu na unachangia katika mapambano muhimu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.