Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yaanza kufikia mabadiliko endelevu ya kidijitali

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwasilisha Tamko la Kisera la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano Duniani (ITU PP 2022) unaofanyika Bucharest, nchini Romania.

Muktasari:

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kuwa Tanzania inatekeleza mfumo wa Taifa wa Uchumi wa Kidijitali, ambao utahakikisha sekta zote za uchumi zinatumia Tehama huku ikiwezesha mabadiliko ya kidijitali yanayojenga jamii jumuishi ya kidijitali kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kuwa Tanzania inatekeleza mfumo wa Taifa wa Uchumi wa Kidijitali, ambao utahakikisha sekta zote za uchumi zinatumia Tehama huku ikiwezesha mabadiliko ya kidijitali yanayojenga jamii jumuishi ya kidijitali kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Waziri Nape amebainisha hayo wakati akiwasilisha Tamko la Kisera la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano Duniani (ITU PP 2022) unaofanyika Bucharest, nchini Romania.

Amesema kuwa Tanzania ina Sera ya Taifa ya Tehama, ambayo imesababisha ongezeko kubwa la matumizi ya Tehama katika sekta mbalimbali za uchumi.

Tanzania pia imewezesha ujumuishaji wa kifedha ambao umehusisha idadi ya watu wa Tanzania ambao hawakuwa wanapata huduma za kibenki hasa jamii ya vijijini.

"Tangu tuanzishe Mfumo wa Leseni uliounganishwa mwaka 2005 ili kuinua TEhama katika jitihada zetu za kuinua ustawi wa kijamii na kiuchumi wa watu wetu, tumeona mafanikio. Shukrani kwa mikakati ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika suala zima la ujumuishaji wa kifedha (Financial Inclusion).

Leo hii kuna zaidi ya watumiaji milioni 35.75 wa huduma za fedha kupitia simu ikilinganishwa na watumiaji milioni 23.34 mwaka 2018" amesema Waziri Nape

Waziri huyo amesema Serikali imewekeza maelfu ya kilomita za Mkongo wa Taifa wa Tehama (NICTBB huku akibainisha kuwa mipango ya uunganishaji wa Mkongo wa Mawasiliano kwa nchi jirani na zisizo na bandari ni ahadi ambazo Tanzania imekuwa ikizipa kipaumbele.

Mkongo wa Taifa unaunganisha nchi zisizo na Bahari kupitia maeneo ya mpakani ya Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia na Malawi. Mkongo huu una urefu wa KM 18,000.

"Ili kupata mitandao ya mawasiliano, mifumo ya habari na upatikanaji wake, Tanzania imeanzisha Timu yake ya Taifa ya Kukabiliana na Dharura ya Usalama wa Kompyuta (TZ-CERT) ili kuratibu matukio ya kimtandao katika ngazi ya kitaifa" ameeleza Nape

Katika kuhakikisha nchi inaunganishwa katika mawasiliano, Tanzania imeanzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USCAF) ambao hadi sasa Mfuko umeweza kuunganisha vijiji 316 vyenye wakazi 730,000. 

"Serikali iliweka malengo mazuri ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma za intaneti yenye kasi na huduma kwa asilimia 80 kitaifa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024" amesema

Waziri huyo amesema usambazaji wa huduma za mawasiliano kwa kila sehemu nchini unaendelea vizuri ili kuziwezesha jamii za vijijini upatikanaji wa simu za mkononi.

Akizungumzia Tanzania kugombea nafasi katika Baraza Kuu la ITU kwa mwaka 2023-2026, Nape amesema uzoefu wa Tanzania katika Sekta ya Mawasiliano unaweza kuwa wa manufaa zaidi kwa familia ya ITU kama mjumbe wa Baraza la ITU hasa katika kipindi hiki ambapo sekta ya mawasiliano inabadilika kwa kasi.

"Napenda kusisitiza kuwa Tanzania imedhamiria kushirikiana na nchi nyingine wanachama, Sekretarieti ya ITU kuifanya ITU kuwa chombo muhimu cha kimataifa ambacho kina mchango mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi zote wanachama" amefanua

Tanzania inagombea kiti cha Baraza Kuu la ITU linalowakilisha eneo D la Afrika ambapo Waziri Nape amewaomba wanachama wote wa ITU waipigie kura Tanzania katika Baraza la ITU, ili iweze kubadilishana uzoefu na familia nzima ya ITU na kuchangia zaidi Dira na Ujumbe wa ITU. 

Amesema Tanzania inashirikiana kwa karibu na ITU kuhakikisha matumizi ya mawasiliano ya simu na Tehama kwa wananchi wote wa Tanzania na msisitizo zaidi kwa wanawake na wasichana, vijana, wazee na watu wenye ulemavu.

Uchaguzi wa baraza Kuu la ITU unatarajiwa kufanyika Oktoba 3, 2022, ambapo Tanzania na nchi zingine 16 zinawania nafasi 13 kuwakilisha bara la Afrika. Baraza hilo lina jumla ya wajumbe 48.