Tanzania yachota Sh45.7 bilioni kupambana na mabadiliko tabianchi

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis

What you need to know:

  • Katika kipindi cha miaka mitano Tanzania imepokea Dola 19.34 milioni kupitia mfuko wa nchi zinazoendelea (Least Development Countries Climate Fund- LDCF).

Dodoma. Katika kipindi cha miaka mitano Tanzania imepokea Dola 19.34 milioni (Sh45.7 bilioni) kupitia Mfuko wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya tabianchi kwa nchi zinazoendelea (LDCF).

 Fedha hizo zilitolea kupitia utekeleza wa miradi mine ambayo inatekelezwa pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala ya Mazingira.

Maelezo hayo yametolewa leo Juni 5, 2023 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Chilo.

Chilo ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa Donge (CCM), Soud Mohammed Jumah ambaye ameuliza kwa miaka mitano iliyopita Tanzania ilipata kiasi gani cha fedha kutoka LDCF.

Naibu Waziri amesema taarifa kwa kina kuhusu miradi yote inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Chilo ameongeza kuwa Serikali itaendelea kutafuta fedha zaidi kutoka kwenye Mfuko wa LDCF ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.