Taylor Swift abeba tuzo ya tatu mfululizo

Tuesday November 24 2020
swift pic
By Mwandishi Wetu

Mwanamuziki wa Pop nchini Marekani, Taylor Swift ameshinda tuzo ya msanii bora wa mwaka ya American Music Award kwa mara ya tatu mfululizo.

Katika kipengele hicho, Swift (30) alikuwa akichuana na mastaa kibao wa muziki kutoka Marekani akiwemo Justin Bieber, Post Malone, Roddy Ricch na The Weekend.

Licha ya kutwaa tuzo kubwa zaidi, Taylor hakufika katika sherehe za kukabidhiwa tuzo hizo zilizofanyika kwenye ukumbi wa The Microsoft jijini Los Angeles na baadaye alieleza kuwa hali hiyo ilitokana na kubanwa na kurekodi nyimbo zake studio.

Tuzo za American Music Awards hufanyika kila mwaka, na mwaka 2020 wasanii waliong’ara kwa kubeba tuzo ukimuacha Taylor Swift ni Justin Bieber, Dua Lipa na Doja Cat ambaye alibeba tuzo ya msanii bora mpya.

Advertisement