Thomas More Machrina: Nidhamu, usimamizi bora wa rasilimali ndiyo misingi ya mafanikio yetu

Thomas More Machrina: Nidhamu, usimamizi bora wa rasilimali ndiyo misingi ya mafanikio yetu

Muktasari:

  • Takribani nyakati zote katika historia ya mwanadamu, elimu imekuwa na manufaa kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii.

Takribani nyakati zote katika historia ya mwanadamu, elimu imekuwa na manufaa kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii.

Leo hii zinapoendelea jitihada za kuhimizana katika ngazi ya familia na Taifa kwamba ni lazima kuwekeza katika elimu, kimsingi sababu kuu ni hiyo kwamba elimu ina manufaa kwa mtu binafsi na kwa jamii.Elimu ni utajiri au mtaji usioweza kuibiwa au kuharibika ambao mzazi/mlezi yoyote anaweza kumpatia mtoto wake.

Elimu ina faida anuwai za kiuchumi na kifedha.Lengo la kumpatia mtoto elimu ni kuhakikisha anapata maendeleo endelevu katika maisha yake ya sasa na baadaye, ili kulinda na kudumisha utu wake pamoja na kuendelea kuimarisha haki zake za msingi hasa za kiuchumi na kuzalisha bidhaa na huduma.

Ndoto ya kila mzazi/mlezi ni kumpatia mtoto wake elimu bora. Haijalishi itagharimu kiasi gani lakini ni suala lisiloepukika kwamba kila mtoto anatakiwa apate elimu bora ili aweze kutimiza ndoto za maisha yake.

Elimu bora ni ile inayoweza kumuandaa mtoto katika mambo makuu matatu; kumuwezesha kuwa na mawazo ya udadisi, uwezo wa kujiendeleza na kujifunza kutokana na vitendo vya wengine na kuvikataa au kuvikubali kulingana na mahitaji yake na jamii kwa ujumla na msingi wa kujiamini katika nafasi yake kama mtu huru na aliye sawa katika jamii yake ili awe na uwezo wa kutatua changamoto zinazomkabili yeye na jamii hiyo katika nyanja nzima ya kiuchumi.

Elimu bora ni lazima izingatie mahitaji ya jamii na kumuandaa mwanafunzi kwenda sambamba na mabadiliko yanayoikumba jamii yake. Ni ukweli usiofichika kwamba ili mtoto wako apate elimu bora lazima umpeleke kwenye shule bora.

Hapa nazungumzia shule zenye uwezo wa kumuandaa mwanafunzi katika misingi niliyoeleza hapo juu.

Katika kuzitambua shule bora za sekondari zilizopo nchini, gazeti hili lilifanya ziara katika shule mbalimbali ili kufahamu ni vitu gani wanafanya vinavyosababisha kuwa bora kitaaluma.

Thomas More Machrina: Nidhamu, usimamizi bora wa rasilimali ndiyo misingi ya mafanikio yetu

Moja ya shule hizo ni sekondari ya Thomas More Machrina iliyopo Mbezi Temboni kwa Msuguri jijini Dar es Salaam. Hii ni kutokana na mwenen-do mzuri wa matokeo ya wanafunzi wake kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha pili, nne na sita. Shule hiyo inaweka mkazo katika kufufua maarifa, kujenga upendo kutengeneza mazingira kwa wanafunzi kupenda kufanya shughuli mbalimbali za mikono.

Historia

Mwanzilishi wa shule hiyo, Profesa Justinian Galabawa anasema Shule ya Sekondari Thomas More Machrina ni shule ya wavulana iliyoanzishwa 2003. Shule hiyo inatoa elimu kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Kipaumbele katika masomo ya hisabati na sayansi.

“Shule ilianzishwa kwa kuzingatia ubia wa Serikali na Sekta binafsi (Public-Private Partnership, PPP) baada ya Serikali kuona kwamba ipo haja ya kuwa na shule za msingi na sekondari zinazomilikiwa na mashirika na watu binafsi, ili kuongeza upatikanaji wa elimu msingi,” anasema Prof Galabawa.

Baada ya kutimiza masharti ya ubia huo, mwaka 2005 shule ilisajiliwa na Wizara ya Elimu kupitia kifungu cha 26 cha sheria ya elimu Namba 25 ya mwaka 1978 kwa namba ya usajili namba; S. 1440. Hivyo shule inafuata sera na mitaala ya Wizara ya Elimu katika utekelezaji wa majukumu yake.

Thomas More Machrina: Nidhamu, usimamizi bora wa rasilimali ndiyo misingi ya mafanikio yetu

Pia shule imesajiliwa kama kituo cha mitihani iliyosajiliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa usajili namba S.1604.Profesa Galabawa anasema awali shule ilisajiliwa kutoa elimu kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne lakini mwaka 2016 ilipata kibali cha kufundisha kidato cha tano na sita kwenye masomo ya sayansi, hivyo kuna michepuo ya PCB, PCM, PGM na CBG.

Matokeo ya mitihani ya Taifa yanaonyesha mafanikio makubwa kwa sababu ya ufanisi katika matumizi ya rasilimali kama; muda, fedha, majengo na walimu.

“Lengo la kuanzisha shule hii ilikuwa sio kupata pesa bali ni hamasa niliyokuwa nayo ndani yangu nikiwa kama Profesa. Moja kati ya vitu ambavyo najivunia ni kuwa na walimu ambao ni wanafunzi wangu wa chuo kikuu na wengi nilikuwa nao tangu shule inaanza mpaka sasa.

Sio kama hakuna matatizo yanayotokea, la hasha! bali huwa tunayageuza kuwa fursa ya kuendeleza shule ,” anasema Prof Galabawa.

Kwa nini nichague kumleta mtoto wangu Thomas More Machrina High School

Prof Galabawa anasema Thomas More Machrina High School imejidhatiti katika kum-fanya mvulana kuwa kijana na raia anayejitambua na kufahamu majukumu yake katika Taifa na jamii inayomzunguka. Wanafunzi wanalelewa katika maadili mema yanayoendana na desturi za kitanzania.

Nidhamu ya kusoma, kufanya kazi za nje, kufanya kazi za darasani ndiyo kitu namba moja tunachokizingatia. Msingi ni nidhamu ya kutumia vitabu na kuvichambua kwa kila somo.

Thomas More Machrina High School elimu ni zaidi ya chombo cha maarifa, bali ni huduma ya ustadi ambayo inahamasisha maisha ya kiroho, nidhamu, kujiamini, kujitambua na maendeleo ya kitaaluma. Pia wanafunzi wanafundishwa kujisimamia wenyewe.

“Tunaamini kwamba kila mwanafunzi ana kipawa ndani yake alichopewa na Mungu ambacho kinahitaji usimam-izi na uangalizi wa karibu ili kuweza kukiendeleza, hivyo tunahakikisha kwamba tunamlea na kumlazimisha mtoto ili aweze kukuza kipawa chake pamoja na kumuongezea uwezo wa kujiamini na kujitambua,” Profesa Galabawa.

Kitaaluma shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani mbalimbali ya kitaifa kwa kidato cha pili, nne na sita. Mfano katika matokeo ya kidato cha pili mwaka 2018, 2019 na 2020 shule ilifanikiwa kutoa daraja la kwanza kwa wanafunzi wote waliofanya mtihani. Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 na 2019 shule ilifanikiwa kutoa daraja la kwanza na la pili na mwaka 2020 shule ilifanikiwa kutoa daraja la kwanza pekee ambapo wanafunzi wote 40 waliofanya mtihani huo walipata daraja la kwanza.

“Shule ilishika nafasi ya kumi kwenye orodha ya shule kumi bora kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016. Pia, tumekuwa tukifanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha sita ambapo katika matokeo ya mwaka 2019 na 2020 shule ilitoa daraja la kwanza, na la pili Hivyo wanafunzi wote walipata nafasi ya kujiunga na elimu ya juu,” anasema Profesa Galabawa.

Thomas More Machrina: Nidhamu, usimamizi bora wa rasilimali ndiyo misingi ya mafanikio yetu

Shule imewahi kutunukiwa tuzo mbalimbali za ubora kama tuzo ya shule bora mwaka 2016 Mkoa wa Dar es Salaam, shule bora ya binafsi mwaka 2013, 2021 Thomas More Machrina imepata tuzo ya shule bora katika shule za sekondari nchini.

“Shule ina mwongozo bora wa ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi na walimu ambao pamoja na mambo mengine unazingatia kumuandaa vyema mwanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa, kuzingatia mazoezi na mafunzo ya vitendo, upatikanaji wa uhakika wa vifaa vya kujifunzia kama vitabu. Kila mwanafunzi ana kitabu chake na mwalimu anatakiwa kuwa na chake wakati wa kufundisha kwa sababu uchambuzi wa maudhui katika vitabu ni sehemu ya mafunzo na ufundishaji,” anasema Profesa Galabawa.

Shule ina maabara za kutosha na za kisasa, malazi bora, chakula bora (wanafunzi wanakula milo minne kwa siku) shule ina mpango maalumu wa lishe kwa wanafunzi, inahamasisha wanafunzi kufanya ibada ili kuimarika kiroho.

Shule ina walimu waliobobea katika ufundishaji na wanafundisha kutokana na taaluma zao, kama ni mtaalamu wa bailojia atafundisha baioloji, vivyo hivyo kwa masomo mengine. Pia walimu wanatakiwa kuwa na stadi za kusimamia maabara. Shule pia imekuwa ikilipa kipaumbele namba moja suala la afya.

Mfano katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona shule iliandaa mkakati wake kupitia mwongozo wa kinga na kuzuia maambukizi katika jamii dhidi ya Covid-19 uliotolewa na Wizara ya Afya.

“Serikali ilipotangaza shule kufungwa, sisi tuliendelea kufundisha kwa njia ya mtandao jambo lililosaidia wanafunzi wetu kuendelea kusoma wakiwa nyumbani, hata hivyo ni changamoto kwetu kwa sababu wazazi ni wagumu kubeba gharama za miundombinu ya mtandao” anasema Mkuu wa Shule hiyo, Constantine Kirwanda.

Matumizi ya Tehama (ICT) katika ufundishaji na usomaji

Makamu Mkuu wa ShuleTaaluma wa shule hiyo, Thomas Ishengoma anasema shule imekuwa na matumizi endelevu ya vifaa vya kielektroniki kama tablets katika kujifunza na kusoma, jambo ambalo linawaongezea umakini na ujuzi katika kusaka maarifa.

Pia inawapa walimu wigo mpana wa kupata maudhui ya kufundishia. Matumizi ya tablets yamewezeshwa na kura-hisishwa kutokana na shule kuunganishwa na mkongo wa Taifa wa mawasiliano ya intaneti kupitia TTCL. Mwalimu Ishengoma anasema gharama za ununuzi wa tablets hizo kwa baadhi ya wazazi ni kubwa.

“Mbali na ufundishaji, shule inatekeleza shughuli mbalim-bali za kitaaluma kama vile; maigizo, debate, klabu za masomo, sanaa za ubunifu, nk. Shule ina mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia,” anasema Profesa Galabawa.

Shule ni kama gereza la mwanafunzi kujifunza, hivyo wanahakikisha wanajenga mazingira mazuri ya kitaaluma na sio ya kukaa na kupiga soga na kupoteza muda. Wanaweka mazingira bora ya nidhamu kuanzia kwa wazazi ili watambue kwamba watoto wanahitaji nini.

“Hatuvumilii vitendo vyovyote vya utovu wa nidhamu katika mazingira ya shule na ikitokea mwanafunzi amefanya kitu kisichoendana na misingi ya shule adhabu kali ikiwemo kufukuzwa shule zinachukuliwa mapema kwa kufuata sheria za nchi. Mfano; kuna wanafunzi wa kidato cha kwanza walimpiga kiranja, baada ya kukaa na bodi tukakubaliana tukawafukuza,” anasema Profesa Galabawa.

Anasema adhabu zote za kinidhamu wanazitoa kwa kufuata mwongozo wa Serikali kama ulivyoelekezwa kwenye sheria ya elimu ya mwaka 1978 na 1995.

Ushirikiano wa shule na Serikali na wazazi

Shule imekuwa na ushirikiano mzuri na Serikali kuanzia ya mtaa mpaka kuu katika mambo yanayohusu uendeshaji wa shule. Pia imekuwa ikihakikisha kwamba sera na miongozo ya elimu iliyopo chini ya Serikali inatekelezwa ipasavyo.Kwa upande wa wazazi shule imeanzisha Chama cha Wazazi na Walimu (PTA) tangu mwaka 2005 ambacho kimesaidia kuwashirikisha wazazi katika masuala mbalimbali ya kitaaluma. Inawashirikisha wazazi kwenye kila kitu kinachohusu maendeleo na motisha kwa walimu na wanafunzi.

“Mbali na ushirikiano huo, pia tunatoa kipaumbele katika maslahi ya walimu na wafanyakazi wengine. Tunahakikisha tunafuata sheria zote za waajiri kama vile haki ya kujiunga na kupeleka mafao katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), bima za afya, kulipa mishahara kwa wakati, kuwapatia motisha nk,” anasema Profesa Galabawa.

Mafanikio na mikakati

Anasema moja kati ya mafanikio wanayojivunia ni wanafunzi wanaomaliza shule hiyo kupata nafasi kwenye vyuo vikubwa ndani na nje ya nchi mfano katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, India, Malaysia, China na Marekani.

Kingine ni kuwawezesha watoto kupata elimu bora inayowasaidia kutimiza ndoto zao pamoja na kuzisaidia jamii zao. Kuwa na wahitimu waliofaulu kwa ubora wa kiwango cha juu wakiwa na nidhamu na maadili mema yanayowasaidia kwenye maisha na kazi zao.

“Tumesaidia kutatua tatizo la ajira kutokana na watu tuliyowaajiri kwenye nafasi mbalimbali, tunalipa kodi kwa Serikali hivyo kuiwezesha kutekeleza mikakati mbalimbali ya kimaendeleo. Tunazalisha wataalamu ambao wanaingia kwenye mfumo wa kusaidia vipaumbele vya Taifa kiuchumi kama vile shughuli za viwanda, afya, uhandisi na kilimo. Mikakati yetu ni kuendelea kuwa bora kwa kupata matokeo mazuri kila mwaka,” anasema mkuu wa shule, Kirwanda.

Kwa mawasiliano zaidi

Shule ya Sekondari Thomas More Machrina

S.L.P 35162 Dar es Salaam

Simu: 0732 9946 45 (General line)    

         0713 518380 (School Administrator)

         0712 63 90 50 (Mkuu wa Shule)

         0713 77 22 88 (Mwanzilishi wa shule)

Barua pepe: [email protected]