TMA yaelezea hali ya joto lililopo

Muktasari:

Mamlaka ya Hewa nchini(TMA) imesema takwimu zinaonyesha kuwa joto la nchi linaendelea kuongezeka kwa kiwango cha juu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka huu ambapo joto la usiku limeongezeka zaidi ikilinganishwa na joto la mchana

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hewa nchini(TMA) imesema takwimu zinaonyesha kuwa joto la nchi linaendelea kuongezeka kwa kiwango cha juu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka huu ambapo joto la usiku limeongezeka zaidi ikilinganishwa na joto la mchana

Mkurugenzu Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi amesema hayo leo Aprili 8, 2020 wakati akitoa ripoti ya tathmini ya hali ya hewa nchini ya mwaka 2019.

Amesema usiku kunatakiwa kuwe na hali ya ubaridi ambapo joto lake linakuwa la chini na mchana kunatakiwa kuwe na joto lakini imekuwa tofauti usiku kumekuwa na joto zaidi.

Amesema kwa wastani joto kubwa kupita viwango vya kawaida ni nyuzi joto 35 limekuwa likiripotiwa katika miezi ya Januari, Februari na Machi hasa katika maeneo mengi ya Kaskazini mwa nchi ambayo ni Pwani ya Kaskazini na maeneo ya nyanda za juu Kaskazini Mashariki.

Amesema ongezeko la joto na ongezeko la matukio ya hali ya hewa mbaya duniani imeathiri nchi yetu kuongezeka kwa joto zaidi hasa usiku ukilinganisha mchana .

"Sekta mbalimbali za uchumi na kijamii waitumie taarifa hii waweze kuweka vizuri mipango ya maendeleo ya nchi yetu kiuchumi na kijamii kama vile kijamii, ujenzi wa viwanda," amesema na kuongeza

 "Tumeona ongezeko la joto linaenda sambamba na kuongezeka kwa matukio ya hali ya hewa mbaya na kuongezeka kwa mvua nyingi katika nchi yetu hivyo wanatakiwa kuchukua taarifa hii," amesema Dk Kijazi.

Amesema sekta hizo zichukue taarifa hiyo na kuiweka katika mipango ya maendeleo endelevu ikiwemo kujenga majengo ya viwanda ambavyo havitaathiriwa na hali mbaya ya hewa ambayo inaweza kujitokeza


Dk Kijazi amesema joto kwa mwaka 2019 ilikuwa nyuzi joto 23.8 sawa na nyuzi joto 0.9, juu ya wastani wa joto wa muda mrefu wa mwaka 1981 hadi 2010 na limechukua nafasi ya nne kuwa joto kali tangu mwaka 1970.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa Dk Ladislaus Chang'a amesema kuwa ripoti hizo zimekuwa zikitolewa tokea mwaka 2011 hafi 2019 kwa lengo la kukuza ufahamj na uelewa kwa jsmiik, wadau na watoa maamuzi juu ys mabadiliko ya hali ya hewa na tsbia ya nchi

 Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, DK Buruhan Nyazi ameipongeza menejimenti ya Mamlaka hiyo kwa kutoa ripoti hiyo kwani ilieleza kwamba ni nchi mbili zinatoa ambayo ni Tanzania na Ivory Cost.