TPDC yaeleza kinachoendelea kitalu cha utafiti wa mafuta

Muktasari:

  • Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeelezea kinachoendelea katika Kitalu cha Eyasi-Wembere chenye ukubwa wa kilometa za mraba 19. 2, kinachopita katika ya mikoa ya Arusha, Manyara, Simiyu, Shinyanga na Tabora.

Dar es Salaam. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limepeleka watalaamu katika Kitalu cha Eyasi-Wembere kwa ajili ya kuweka vifaa chini ya ardhi ili kuchukua taarifa za viashiria vya upatikanaji wa mafuta (Oil sea).

 Kitalu cha Eyasi Wembere chenye ukubwa wa kilometa za mraba 19. 2, kinapita katika ya mikoa ya Arusha, Manyara, Simiyu, Shinyanga na Tabora.

“Kazi hii itafanyika kwa miezi miwili baada ya hapo watapeleka maabara kwa ajili ya kuangalia je kuna viashiria vya mafuta kweli au mafuta yenyewe,” amesema Samwel Magambo, Mjiolojia kutoka Idara ya Mkondo wa Juu wa shirika hilo.

Magambo amesema hayo leo Jumatano, Agosti 3, 2022 katika siku ya kwanza la Kongamano la Kimataifa la Nishati 2022, linalofanyika jijini Dar es Salaam.

“Viashiria vikipatikana huwezi kujua kiwango kilichopo, kazi ya maabara hiyo inaweza kuchukua mwezi mmoja au miwili.”

Kauli hiyo ameitoa leo katika Kongamano la Kimataifa la Nishati 2022 lililokutanisha kampuni 100 za kigeni na washiriki zaidi ya 1000 wakiwamo wawakilishi 300 kutoka mataifa 25 duniani.

Katika ufafanuzi wake, Magabo amesema TPDC imeshatangaza zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi atakayefanya kazi ya kuchukua, kuchakata na kutafsiri data za mtetemo kutoka kwenye kitalu hicho. Amesema lengo ni kutambua maeneo ya kuainisha visima virefu katika kitalu hicho.

Kabla ya kufikia hatua hiyo, TPDC ilifanikiwa kuchukua taarifa za kijiolojia(AGG Data) ziliotafsiriwa na kuonyesha sifa ya miamba tabaka yenye uwezo wa kuzalisha mafuta. Pia kati ya 2019 hadi 2020 ilichimba visima vitatu vifupi ili kujua mpangilio wa miamba