Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA Moshi kuwakamata wasiotoa, dai risiti za EFD

Muktasari:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kilimanjaro imesema kuanzia Februari Mosi, mwaka huu, itaanza kampeni maalumu ya" Kamata wote"kwa asiyetoa na asiyedai risiti za mashine za EFD.

Moshi. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kilimanjaro imesema kuanzia Februari Mosi mwaka huu, itaanza kampeni maalumu ya "Kamata wote" kwa asiyetoa na asiyedai risiti za mashine za EFD.

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 28, 2022 na Ofisa msimamizi wa kodi Mkoani hapa, Odupai Papaa ambapo amesema ukaguzi huo utafanyika katika mitaa yote ya mkoa huo.

Taarifa hiyo imesema kuwa muuzaji ambaye hatatoa risiti atatozwa faini ya Sh3 milioni hadi Sh4.5milioni na mnunuzi ambaye atakutwa na bidhaa isiyo na risiti faini yake ni Sh30, 000 hadi Sh1.5 milioni.

"Kuanzia tarehe 1, Februari, 2022 itaanza kampeni maalumu ya "Kamata wote"ya asiyetoa na asiyedai risiti  ya EFD,"ukaguzi utafanywa katika mitaa yote ya Mkoa wa Kilimanjaro,"

"Muuzaji akikamatwa hajatoa risiti faini yake ni Sh3Milioni hadi Sh4.5milioni na mnunuzi akikutwa na bidhaa isiyo na risiti faini yake ni Sh30, 000 hadi Sh1.5 milioni,"