Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trilioni tisa kulipa deni la Serikali

Trilioni tisa kulipa deni la Serikali

Muktasari:

Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge kuidhinisha Sh14.94 trilioni bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 huku Sh9.09 trilioni zikienda katika kulipa deni la Serikali.

Dodoma. Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge kuidhinisha Sh14.94 trilioni bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 huku Sh9.09 trilioni zikienda katika kulipa deni la Serikali.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba ameyasema hayo leo Jumanne Juni 7, 2022 wakati akiwasilisha mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Dk Mwigulu amesema kati ya kiasi hicho, Sh13.62 trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh1.32 trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Aidha, Dk Mwigulu amesema katika mwaka 2022/23, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini (TADB) imepanga kutoa mikopo ya Sh78 bilioni kwa sekta ya viwanda, hususani viwanda vya mafuta ya kula na sukari katika Mkoa wa Kigoma, Shinyanga na Manyara.

“Mikopo hiyo inatarajia kupunguza upungufu wa mafuta ya kula na sukari hapa nchini,”amesema Dk Mwigulu.

Aidha, amesema benki imepanga kutoa mkopo wa takribani Sh130 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa pamba na kahawa.