Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tughe yazungumzia migogoro, migomo kazini

Mwenyekiti wa Chama Cha wafanyakazi wa Serikali na Afya(TUGHE) Taifa Archie Mntambo, wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano Mkuu wanachama hicho mkoani Morogoro,ambapo amesema Ni vyema Vijana wakajitokeza katika masuala ya Uongozi.

Muktasari:

Mkutano mkuu Chama cha wafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe) nchini Tanzania unafanyika mkoani Morogoro ukihusisha wanachama wa chama hicho kutoka nchi nzima.

Morogoro. Katibu mkuu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe) Henry Mkunda amesema waajiri wasionekane maadui mahala pa kazi badala yake wawe washirika kwenye mambo ya uhusiano kati ya mfanyakazi na mwajiri mwenyewe.

Aidha katibu huyo amesema masuala ya migogoro na migomo maeneo ya kazi hayana nafasi wala tija hivyo vyama vya wafanyakazi viendelee kufanya majadiliano kila wakati.

Amesema hayo leo Alhamisi Desemba 19, 2019 wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho unaoendelea mkoani Morogoro ulioshirikisha wajumbe wa mkutano huo kutoka mikoa yote nchini Tanzania.

Amesema Tughe itaendelea kufanya ushawishi wa kuhakikisha maeneo ya kazi yanakuwa salama na mahala ambapo hakuna matawi yaweze kuanzishwa mara moja huku wakiendelea kushawishi wanachama kujiunga katika chama hicho.

“Tumeelekezwa chama kiendelee kushirikiana nao, mambo ya migomo hayana tija wala nafasi isipokuwa tusonge mbele tukutane na waajiri tukutane nao kwenye meza ya pamoja na tujadiliane nao,” amesema.

Amesema kuwepo kwa mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi inasaidia na kutoa nafasi kwa wafanyakazi kuweza kushiriki mchakato wa uamuzi wa taasisi na kwa mambo ambayo yanawagusa wao moja kwa moja.

Naye Mwenyekiti wa Tughe, Archie Mntambo ameeleza umuhimu wa vijana kujitokeza kwenye uongozi wa nyanja mbalimbali kwa kuwa hao ndiyo watakuwa viongozi kwa siku zijazo na kwamba lazima waendelee kuhamasishwa katika kushika nafasi za uongozi.

Mwenyekiti wa Wanawake Tughe, Dk Jane Madete amesema kwa sasa changamoto za wanawake makazini zimekuwa zikiendelea kupungua kila mara na kuwapo kwa matawi sehemu za kazi imesaidia kwa mapana makubwa kutatua migogoro  mbalimbali iliyokuwa ikiwakabili.