Ubalozi wa Uswisi na FSDT kuzindua utafiti kwa vijana vijijini

Mkurugenzi Mtendaji wa FSDT, Sosthenes Kewe

Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, Ubalozi wa Uswisi (Switzerland) kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), watazindua utafiti wa Huduma jumuishi za fedha kwa Vijana wa Vijijini katika hafla itakayofanyika kwa njia ya mtandao saa 8 mchana.

 Utafiti huo unalenga kusambaza maarifa ya kina kuhusu tabia na changamoto za vijana wa vijijini nchini Tanzania hususani wasichana,wenye umri wa miakakati ya 16 na 24 katika masuala ya fedha.

Taarifa ya FinScope Tanzania ya mwaka 2017 ilibainisha kuwa wanawake na wanaume wa vijijini wenye umri kuaziamiaka 16 hadi 24 waliokadiliwa kufikia  takriban watu milioni 4.4 walikuwa sehemu ya idadi ya watu waliotengwa katika huduma za fedha, huku asilimia 45 wakiwa hawajachukua huduma yoyote ya fedha rasmi au isiyo rasmi.

Utafiti wa Fedha jumuishi kwa Vijana wa Vijijini unaonyesha wasifu halisi wa vijana wa vijijini ili kuwezesha ubunifu wa bidhaa au huduma zinazolenga kundi hili la soko linalojitokeza. Inachunguza zaidi mahitaji, mtamanio na hali ya sasa ya kiuchumi ya vijana wa vijijini, na jinsi mawasiliano ya sasa na mikakati ya watoa huduma za fedha kuingia sokoni, mipango ya uwezeshaji vijana na sera mbalimbali zinavyowaakisi.

“Mfuko wa Kuendeleza sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) walibainisha kuwa Vijana wa Vijijini ni kundi muhimu sana katika kuleta mabadiliko kupitia huduma jumuishi za fedha, hivyo ushirikiano baina yake na Ubalozi wa Uswisi umewasilisha fursa nzurikuimarisha uelewa wa ndani wa kundi hili”, alisema Sosthenes Kewe ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa FSDT

Utafiti huu unataka kutarifu mikakati ya maendeleo ya uchumi kwa vijana wa vijijini, huduma za fedha na mikakati inayolenga kuongeza ajira kwa vijana wa vijijini kwa kujiajiri kupitia huduma za fedha jumuishi zilizoboreshwa. Utafiti wa Vijana ulitumia jicho la jinsia katika  taarifa nzima kubainisha changamoto na fursa mahususi zilizopo kwa ajili ya mwanamke wavijijini.

“Kuongeza huduma jumuishi za fedha kwa vijana  vijijini ni changamoto kubwa – na kuongeza huduma jumuishi za fedha kwa vijana wadogo wa kike vijijini ina umuhimu wa kipekee kwani hawajanufaika kiusawa. Utafiti huu unachunguza kiini cha tofautiza usawa  wa kijinsia unaozuia kuwajengea uwezo wanawake”, alisema Balozi wa Uswisi Didier Chassot.

“Upatikanaji na matumizi ya  bidhaa na huduma bora za fedha ni muhimu kwa ukuaji wa  uchumi jumuishi na katika kupunguza umasikini”. 

Tukio hili litasambaza ufahamu unaoweza kufanyiwa kazi kutokana na utafiti uliolenga kutatua changamoto mbalimbali zinazolikumba  kundi lengwa la vijana. Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, tukio hilo litazingatia hasa wasichana. Utafiti wa Fedha jumuishi kwa Vijana Vijijini ulifanywa na taasisi ya  IPSOS kwa kushirikiana na Fundacion Capital.

Uswisi imekuwa ikiunga mkono miradi ya pande mbili na ile ya kikanda nchini Tanzania tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960.

Mwaka 1981, Tanzania ikawa nchi ya kipaumbele kwa misaada rasmi ya maendeleo kutoka nchi ya Uswisi na inaendelea kupokea takriban $ 22 kila mwaka.

Mpango wa Ushirikiano wa Uswisi nchini Tanzania 2021 - 24 unalenga kuwawezesha vijana, hasa wasichana masikini, kuendelea kijamii na kiuchumi.

Mfuko wa Kuendeleza sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) ni taasisi inayo jihusisha na ujenzi wa masoko wezeshi kwa kusaidia kutatua vikwazo na changamoto zilizoko sokoni na kuchagiza ukuaji wa sekta ya fedha inayolenga  kupunguza hali ya umaskini wa watu na kipato