Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uchakachuaji mbolea sawa na uhujumu uchumi, sheria yaja

Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Dk Stephan Ngailo

Muktasari:

  • Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema itakuja na sheria itakayowahesabu wafanyabiashara wanaochakachua mbolea kama wahujumu uchumi.

Iringa.  Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imepiga marufuku kwa mfanyabishara yeyote kufanya uchakachuaji wa mbolea, huku ikiandaa sheria itakayowatambua wenye kufanya uharifu huo kama wahujumu uchumi.

Katika msimu wa kilimo uliopita baadhi ya wafanyabiashara walibainika kuchakachua mbolea kwa kuchanganya na mchanga jambo linaloathiri ukuaji wa mazao.

Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Dk Stephan Ngailo ameiambia Mwananchi, leo June 7, 2023 kuwa wanaenda kuboresha sheria ili badala ya kulipa faini, atakayebainika kufanya kosa hilo ashtakiwe kwa kosa la uhujumu uchumi na adhabu yake iwe kifungo.

“Uchakachuaji ni ukatili na uuaji, atakayebainika kwa jinsi yeyote ile adhabu yake iwe kali na isiwe faini bali kifungo moja kwa moja,” amesema Dk Ngailo.

Kulingana na TFRA, wanaendelea kusimamia udhibiti, ukaguzi na ubora wa mbolea kuanzia ngazi ya awali kiwandani au bandarini mpaka kwa walaji wa mwisho.

“Mwaka huu kuanzia Julai 1, 2023 wataweka wawakilishi kwenye kila mkoa kwa ajili ya kuratibu na kusimamia suala la mbolea. Niwaombe wakulima wakiona jambo lisilo la kawaida wapige simu 0733 800 200, tuachukua hatua stahiki,” amesema Dk Ngailo.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima walisema mbolea iliyochakachuliwa imekuwa mzigo mkubwa kwao kwa sababu, wakishanunua sio rahisi kuitambua.

“Fikiria unanunua mbolea kumbe imechanganywa na mchaka, ikienda kukuzia au kupandia huoni faida yoyote ile. Hii ni hatari sana kwa ukuaji wa mazao,” amesema Joseph Kilasi, mkulima wa mahindi.

Aliishauri TFRA kuweka mkakati wa kuhakikisha wanapita kwenye magodauni ya mawakala ili wafanye ukaguzi na kuwakamata mawakala wasio waaminifu ambao kwa nia mbaya wanadidimiza kilimo.