Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujumbe wa Krisimasi

Muktasari:

  • Watanzania wameungana na Wakristu wengine duniani kusherehekea sikukuu ya Krisimasi huku katika ibada kwenye makanisa mbalimbali nchini ujumbe kuhusu amani, kuonea huruma wasionacho, kujikinga na ugonjwa wa Uviko-19 vikitawala.  



Dar/mikoani. Watanzania wameungana na Wakristu wengine duniani kusherehekea sikukuu ya Krisimasi huku katika ibada kwenye makanisa mbalimbali nchini ujumbe kuhusu amani, kuonea huruma wasionacho, kujikinga na ugonjwa wa Uviko-19 vikitawala.  

Mkoani Tabora Askofu mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora,Paul Ruzoka amesema, "sikukuu ya noel ina sifa kubwa ya kujenga matumaini ya jambo ambalo ukilipata unafurahi. Wakristo wanapaswa kumshukuru Mungu kwa mema aliyowatendea na hata yale mazito waliyokumbana nayo.”

Huku akisisitiza uvumilivu kwa wote waliopoteza ndugu na jamaa mwaka 2021 akiwemo Hayati John Magufuli amesema, “kwa lile la kwanza la kuondokewa na wapendwa wetu tunapaswa kubaki na matumaini na kumkiri Yesu ni Mungu, tukitafakari yaliyopita na kutoishi kwa hofu kwani Mungu ndiye tumaini letu na tumpe sifa na utukufu.”

Naye Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika,  Dk Dikson Chilongani aligusia suala la wamachinga  akiwataka viongozi kutambua matatizo wanayoyapitia.

Siku za hivi karibuni wamachinga wameondolewa katika maeneo yasiyo rasmi na kupelekwa katika maeneo waliyotengewa jambo ambalo limekuwa na maoni tofauti kutoka kwa watu wa kada mbalimbali.

Katika maelezo yake Askofu Chilongani amesema kuna baadhi ya viongozi wanatoa maagizo wakiwa kwenye viti vyao vya enzi bila kujua walio chini wana matatizo gani.

Akihubiri katika ibada ya Krismasi kwenye  Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu amesema, “sina uhakika kama kweli baadhi ya viongozi wanajua hali ya maisha ya wamachinga, wao wanatoa magizo wakiwa kwenye viti vyao vya enzi, hiyo siyo sifa ya kiongozi, wanatakiwa kushuka chini ya kujifunza maisha ndipo watoe maagizo.”

Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Patrick Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe, Padri Dennis Hula amesema, “jamii ishikamane katika sikukuu hii iwe kama watoto wadogo wasiokuwa na tamaa za mali na mwili,  Wakristo tuondoe tamaa ndani ya mioyo yetu ambayo ndiyo chanzo cha maovu na mafarakano.”

Amesema familia nyingi zimekuwa na  mzozo wa kupata mahitaji ya mavazi ya sikukuu lakini isiwe chanzo cha ugomvi na kama yapo basi sikukuu itumike kujitafakari na kufanya upatanisho.

Askofu wa Kanisa la EAGT Jimbo la Vwawa ,  Patsoni Mwazembe amesema watu wengi katika kipindi hiki cha sikukuu wanafikiria kusherehekea   kwa matendo mbalimbali yakiwepo na yale yanayoenda kinyume na maadili ya dini kama vile uzinzi na ulevi.

Amesema Wakristo wanatakiwa kujua maana ya Krisimasi kwamba si siku ya kutenda matendo maovu bali kutenda matendo mema kama  kuwasaidia masikini na kusali.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo amesema ni wajibu wa Kila mmoja kuitumia sikukuu ya Krisimasi kutafuta amani na furaha kwa wengine na kuepuka kuwasababishia watu huzuni na uchungu.

Askofu Shoo ambaye pia ni mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya kanisa hilo amebainisha kuwa  wapo wanasababisha huzuni na uchungu kwa wengine kwa sababu tu wana nafasi, nguvu na mamlaka na kuwataka kuepuka hali hiyo.

"Ni kweli yapo mambo yanayoendelea katika jamii na nchi yetu, wapo watu wanaosababisha wenzao wakose amani, wamewasababishia maumivu na uchungu moyoni, maumivu ambayo yamegusa hata familia za hao wenzetu, wamefanya hivyo kwa sababu tu wanayo nguvu, wana nafasi na wana mamlaka."

"Kwa neema ya Mungu tumejaliwa kuiona Krisimasi nyingine ya mwaka huu, sote tunajua tulikopitishwa na tulikopitia tangu Krisimasi iliyopita hadi kufikia siku hii ya leo, hii ni sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutupa uzima na afya. Badala ya kunyimana amani tutakiane furaha, badala ya kusababishiana uchungu na machozi, tusababishe amani kwa watu wote, tuombe Mungu atupe neema ya kuumaliza mwaka huu kwa amani na kuuanza mwaka 2022 na ukawe mwaka wa Baraka,” amesema.

Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dk Solomon Massangwa amesema Watanzania hawapaswi kuwa na hofu ya ugonjwa wa Uviko-19 bali wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari.

"Kwa Yesu tunajifunza kutoogopa,  amekubali kuacha enzi akazaliwa mahali ambapo anaweza kuambukizwa tetenas kwa hiyo hata kama corona ipo ukiwa karibu na Mungu uhitaji kuogopa bali kuchukua tahadhari zote za kujikinga ikiwemo kupata chanjo.”

“Kristo amezaliwa kwa ajili ya watu wote ndio maana anaitwa Emmanuel hutuhitaji kuogopa kitu chochote ni kitu gani kinakuogopesha,  kukosekana kwa mvua, corona, njaa, biashara kushindwa kurudisha mkopo au nini? Usiogope,” amesisitiza.

Askofu wa Kanisa la Bethlem Gospal Revival Church, Edward John amesema, “nyakati hizi zilitabiliwa…, nyakati za hatari ikiwemo watu kuuana ,ndoa kuvunjika na wengine kujinyonga kwa mitazamo huo Yesu yupo karibu kuja hivyo wanatakiwa kumuangukia Mungu ili wasiingie kwenye majaribu kama haya.”


Robert Kakwesi (Tabora), Habel Chidawali (Dodoma), Stephano Simbeye (Songwe), Pamela Chilongola (Dar), Florah Temba na Janet Mushi (Moshi),