Ukiona dalili hizi tambua injini ya gari lako ina shida

Injini ni moyo wa gari, inalipa gari nguvu inayohitaji kufanya kazi kwa usahihi. Wakati injini imeharibiwa, itaathiri vibaya utendaji kazi wa gari lako.

Kwa bahati nzuri, unaweza kujiokoa kutotumia pesa nyingi kwa kugundua haraka shida ya injini ya gari lako kabla ya kusababisha athari mbaya.


Taa ya “check engine” kuwaka

Hii ni taaa inayowaka kwenye dashboard ili kumpa tahadhari dereva wa gari kuwa injini ina shida na inapowaka usipuuza wahi haraka kwa fundi wako kaangalie tatizo ni nini kuepusha hasara.

Taa hii inaweza kuwaka endapo oxygen sensor inahitaji kubadilishwa, mass airflow sensor inahitaji kubadilishwa, catalytic converter imeharibika na inaitaji kurekebishwa, plug zimechoka nk.

Gari kuwa na mlio usio wa kawaida

Ukisikia mlio wa knock unatoka ndani ya boneti basi ujue injini inakaribia kufa. Mlio katika injini unaweza sababishwa na piston, bearing na vipuli vingine vya ndani hivyo ukisikia mlio usio wa kawaida wahi haraka kwa fundi.

Kupuuzia tatizo hili linaweza kuja kukuingiza kwenye gharama kubwa ya kununua injini nyingine hivyo basi kuwa makini.


Gari kuwa na “miss”

Gari kupata “miss” kuna sababishwa na sababu mbalimbali kwa hiyo unapoona tatizo hili wahi kwa fundi wako akaangalie kama ni spark plug zibadilishwe, coil ama pump ya mafuta. Yote haya ni yakuangalia ili injini iwe na maisha marefu. 


Gari kuvuja oil kwenye injini

Ukiona kuna mgando wa oil chini ya gari, tambua maisha ya injini yako sio marefu, hii yote inasababishwa na oil kuvuja kwenye na   kufanya oil kupungua na msuguano wa piston kuzalisha joto kali la vyuma na kukosa kilainishi kinachoweza punguza msuguano wa piston.

Oil inayovuja inaweza kwenda mpaka kwenye throtal body na kuziba mifumo ya hewa kwenye gari hivyo kuwa makini sana.

Kusikia harufu ya oil ndani ya gari yako

Ikifika hatua harufu inasikika ndani ya gari tambua maisha ya injini yako hatarini. Harufu kali kutoka kwenye exose sio dalili nzuri kabisa hivyo usiipuuze nenda kwa fundi wako akuangalizie shida ni nini.


Gari kuongeza ulaji wa mafuta

Mara nyingi injini inapokuwa na shida ulaji wa mafuta huwa una badilika kabisa hivyo ukiona ulaji wa mafuta sio mzuri nenda kwa fundi kaangalie shida nini.


Injini kukosa nguvu

Hili liko wazi, unapoona injini inakosa nguvu hata kupandisha mlima mdogo basi jua kuna tatizo na jitahidi kuwahi mara moja kwa fundi.


Rangi ya moshi kutoka kwenye exose

Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza sababisha injini kutoa moshi. Kupitia hili, rangi ya moshi itakupa jibu kamili kuwa gari lina shida gani.

Ukiona moshi ni mweusi ujue injini haifanyi “combustion” vizuri hii hupelekea kuchoma mafuta mengi na inaweza sababishwa na kuharibika kwa “fuel injectors”, air filter nk. Hivyo basi ukiona kuna shida wahi mapema kwa fundi ujue tatizo.

Kama kuna dalili nyingine ususite kutuandikia kupitia namba za simu zilizopo juu ya ukurasa huu.