Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upatikanaji wa fedha EAC wafikia zaidi ya Sh190 trilioni

Katibu wa EAC, Veronica Nduva akizungumza kwenye mkutano huo.

Muktasari:

  • Mikopo ya uwekezaji iliyotolewa na sekta za kibenki katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeongezeka kutoka Dola 60 bilioni (Sh142.5 trilioni) Juni 2023 hadi Dola 66.6 bilioni  (Sh158.2 trilioni) Juni 2024.

Arusha. Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uwekezaji, mikopo na miamala katika nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) umeongezeka kutoka Dola za Marekani 74 bilioni (Sh175.7 trilioni) mwaka 2023 hadi kufikia Dola 81.7 bilioni (Sh194 trilioni) mwaka 2024.

Mbali na hilo, jumla ya mikopo ya uwekezaji iliyotolewa na sekta za kibenki katika nchi za EAC imeongezeka kutoka Dola 60 bilioni (Sh142.5 trilioni) Juni 2023 hadi Dola 66.6 bilioni  (Sh158.2 trilioni) Juni 2024.

Hayo yamebainishwa Desemba 11, 2024 na Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva wakati akizungumza na wataalamu wa fedha, biashara na uchumi kutoka sekta binafsi na umma na asasi za kiraia (CSO’s) kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Kulikuwa na ongezeko la usambazaji wa fedha za EAC kutoka Dola 74 bilioni Juni 2023 hadi Dola bilioni 81.7 Juni 2024. Hii inaashiria fedha zaidi zinapatikana kwa miamala, mikopo na uwekezaji.”

Amesema takwimu hizo zinapaswa kuhimiza wanajumuiya kuongeza juhudi katika kufanikisha muunganiko wa sarafu ya pamoja (single currency) na kutoa suluhisho la malipo ya mpakani yaliyoshirikishwa kwa haraka.

Amesema kwa upande wa EAC, wanaendelea na jitihada kuelekea umoja wa fedha ambayo imeahirishwa tena hadi mwaka 2032 kutoka mwaka 2030 waliokuwa wamekubaliana.

“Ingawa muda wa kufanikisha hilo ulirekebishwa hadi mwaka 2032, hatua muhimu zimepigwa katika utekelezaji wa ramani ya njia ya sarafu moja na tunatazamia kufikia hitimisho la taratibu za uanzishaji wa taasisi zinazohitajika,” amesema.

Amesema maendeleo na matumizi ya mfumo wa malipo wa Afrika Mashariki yanabakia kuwa kipaumbele cha juu na mazungumzo kuhusu muunganiko wa sarafu unaendelea kutawala mijadala yao.

Nduva pia amesema jumuiya inaendelea kupiga hatua kubwa hasa uoanishaji wa sera za biashara unaoendelea kuwa kipaumbele cha kimkakati.

Amesema sera hizo zinalenga kuondoa ushuru wa ndani na vikwazo visivyo vya ushuru kuwa endelevu katika kuzidi kukuza biashara ndani ya EAC na nje.

“Matunda ya juhudi zilizofanywa yanaonekana kupitia ongezeko la biashara ndani ya EAC na kuimarisha ushirikiano wetu zaidi ambapo kulikuwa na ongezeko la asilimia 12.6 katika biashara ndani ya EAC kutokana na juhudi za kuondoa vikwazo vya kikodi na visivyo vya kikodi mwaka 2023,” Amesema.

Kwa upande wa Vituo vya Pamoja vya Mipaka (OSBPs), Nduva amesema vimeboresha taratibu za forodha ili kupunguza muda wa kuvuka mipaka na wamefanikiwa kwa asilimia 70 na kuzalisha akiba ya zaidi ya dola 63 milioni kwa mwaka.

“Juhudi hizi zimezaa matokeo mazuri katika biashara ya kikanda. Biashara ndani ya EAC ilikua kutoka dola 6.2 bilioni mwaka 2017 hadi dola 13.8 bilioni mwaka 2023.

Na biashara na ulimwengu mzima pia iliongezeka kutoka dola 65.3 bilioni mwaka 2017 hadi dola 109.4 bilioni mwaka 2023,” ameongeza.

Biashara kati ya EAC na Afrika, Nduva amesema imeongezeka kutoka dola 19.4 bilioni mwaka 2017 hadi dola 24.4 bilioni mwaka 2023, ikichochewa na ushiriki katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Nduva alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuwa na matumizi bora ya rasilimali muhimu kwa ujumuishaji wa kikanda kwa manufaa yao binafsi na EAC kwa ujumla.

Zaidi ameipongeza rekodi safi ya ukaguzi wa hesabu za EAC na usimamizi wa fedha na kuitaka Jumuiya kuimarisha uwazi na ushirikishwaji wa wananchi kupitia majukwaa mbalimbali ya kikanda.

Katika mkutano huo wa siku tatu unatoa jukwaa kwa wadau wa sekta za umma na binafsi kubadilishana uzoefu na kupendekeza suluhisho ya changamoto zinazoikumba EAC hasa za kiuchumi, afya, miundombinu na biashara.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Ofisa Mkuu wa Utumishi wa Umma kutoka Ofisi ya Rais wa Kenya, Felix Koskei amesema maoni ya wadau hao yatalenga kuboresha ujumuishaji wa kiuchumi na maendeleo ya kijamii, amani na usalama wa kikanda, maendeleo ya Katiba ya muungano wa kisiasa wa EAC na marekebisho ya Mkataba wa EAC ili kuhudumia EAC iliyopanuka zaidi.

Amesisitiza dhamira ya Rais William Ruto, kama mwenyekiti mpya wa mkutano wa wakuu wa nchi za EAC, ya kuelekeza kanda hiyo katika kuimarisha ujumuishaji wa kiuchumi na kijamii.

Amesema uwajibikaji kwa wananchi na matumizi bora ya rasilimali ni muhimu kwa ujumuishaji wa kikanda.

Pia, amepongeza rekodi safi ya ukaguzi wa hesabu za EAC na usimamizi wa fedha, aliitaka jumuiya kuimarisha uwazi na ushirikishwaji wa wananchi kupitia majukwaa mbalimbali ya kikanda.