Ushuru katika korosho wakwamisha pembejeo

Muktasari:

Wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitarajiwa kukutana na wadau kujadili maendeleo ya korosho, Wizara ya Kilimo imesema imebuni mfumo mbadala wa kupeleka pembejeo kwa wakulima.

Mtwara.

Mtwara. Wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitarajiwa kukutana na wadau kujadili maendeleo ya korosho, Wizara ya Kilimo imesema imebuni mfumo mbadala wa kupeleka pembejeo kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda alisema wanatarajia kuongeza mavuno mwaka huu, ndio maana Serikali inapeleka pembejeo bure kwa wakulima.

“Mpaka sasa asilimia 30 ya wakulima wamepata pembejeo muhimu wanazozihitaji. Tumezihusisha benki za biashara na kampuni binafsi kufanikisha hilo,” alisema.

Profesa Mkenda alitoa maelezo hayo jana, alipoulizwa kuwa, Serikali inamsaidiaje mkulima wa korosho asiyeweza kumudu gharama za pembejeo baada ya kuhamisha mapato yote ya kuuza bidhaa nje ya nchi (export levy) kwenda mfuko mkuu wa hazina, hivyo wakulima kujitegemea kwa mapato.

Mwaka 2018 Serikali ilihamisha zaidi ya Sh200 bilioni zitokanazo na tozo hiyo ya kuuza mazao nje ya nchi zilizokuwa zinatumika kusambaza bure pembejeo kwa wakulima, hali iliyoshusha uzalishaji.

Kabla ya uamuzi huo wa Serikali, msimu wa mwaka 2017/18 tani 313,826 zilivunwa ambazo ni nyingi zaidi miaka ya hivi karibuni, lakini uamuzi huo uliofanywa na kuridhiwa na Bunge, umeporomosha uzalishaji.

Katika msimu wa mwaka 2018/19 mavuno yalipungua hadi tani 225,154 na zikafika tani 206,719 mwaka jana.

Mavuno hayo ya msimu wa mwaka 2017/18 yamepungua baada ya kupanda kutoka 265,238 zilizovunwa msimu wa mwaka 2016/17 na zilipanda kutoka tani 155,245 za msimu uliotangulia.

“Wakulima hawapati pembejeo na kangomba imezuiwa, wanapataje fedha ya kununua dawa? Serikali haikuwa na sababu za msingi sana kuzishikilia fedha hizo, hasa ikizingatiwa korosho ndio zao pekee linalotozwa kodi ya usafirishaji nje,” alisema Mbaruku Muhiddin, mkulima wa korosho wilayani Masasi.

Waziri wa Kilimo alisema wamekisikia kilio cha wakulima hao na baada ya kutafakari wakaandaa utaratibu wa kupeleka pembejeo kwa wakulima hao bure.

“Kuna kampuni saba za pembejeo mpaka sasa zinazofanya kazi kwa karibu sana na vyama vya ushirika kuhakikisha kila mkulima anapata kiasi kinachomtosha,” alisema Mbaruku Muhiddin.

Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa fedha hizo kurudishwa kwenye mfuko wa Bodi ya Korosho ili zitumike kama zilivyokusudiwa alisema, “kwa kuwa mabadiliko yalifanywa na Bunge, mchakato wake ni mrefu kidogo.”

Wakati Profesa Mkenda akieleza mikakati na hatua ambazo wizara yake imechukua, kikao cha Waziri Mkuu kitakachofanyika mjini Lindi kinatarajiwa kuwahusisha wakuu wa mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Pwani na Lindi, viongozi wa vyama vikuu vya ushirika, Bodi ya Korosho Tanzania na wadau wengine muhimu.

Ajenda kubwa ya kikao hicho ni kujadili suala la pembejeo za korosho zinazoendelea kusambazwa.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack alisema Majaliwa atapokea taarifa ya mgawanyo wa pembejeo uliofanywa hadi sasa.

Zainab alisema hadi sasa pembejeo za maji zimesambazwa kwa zaidi ya asilimia 90 ila hana takwimu za dawa ya sulphur inayoendelea kusambazwa na kampuni ya Bajuta International, Benz Agro Star, Prosperity Agro Star, Suba Agro na JM Traders.

“Nadhani tunakwenda kujadili suala la pembejeo na maendeleo ya korosho kwa jumla kwa vile sisi ndio wadau wa zao hili kwa mikoa yetu hii,” alisema Mohamed Mwinguku, meneja mkuu wa Chama Kikuu cha ushirika Tandahimba na Newala (Tanecu).

Sehemu ya barua ya mwaliko ambayo wadau wanaoshiriki mkutano huo unaoandaliwa na Bodi ya Korosho wametumiwa inasema utafanyika katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Katika msimu wa korosho kwa mwaka huu, vyama vikuu vya ushirika vyote kwa pamoja vimekubaliana kwamba Chama Kikuu cha Ushirika Masasi Mtwara (Mamcu) ndicho kitaingia mkataba wa kusambaza pembejeo wenye thamani ya Sh59.6 bilioni.

Pembejeo hizo ni lita milioni 1.372 za viuatilifu vya maji na tani 21,000 za sulphur (salfa).

Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao, Nurdin Said Swallah alisema atashiriki kikao hicho na kutoa maoni yake kuhusu kero zinazowahusu wakulima wa korosho wa Lindi na mikoa mingine 17 inayolima zao hilo.

“Kilimo kinaajiri watu wengi na korosho ni miongoni mwa mazao ya kimkakati. Tukiondoa changamoto zilizopo, maisha ya wakulima wa kanda ya kusini yataimarika,” alisema Swallah.