Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UVCCM kuingia shambani kuwatia moyo vijana mradi wa BBT

Katibu Hamasa na Chipukizi, Edna Lameck (kushoto) akikabidhiwa ofisi ya Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Upanga, Dar es Salaam na  Burugu Majenge aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo.

Muktasari:

  • Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) amekabidhiwa ofisi rasmi leo, Aprili 14, 2023.

Dar es Salaam. Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) unatarajia kuanzisha utaratibu wa kukutana na kuzungumza na vijana mara kwa mara kuhusu changamoto zinazowakabili.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Saaam, Ijumaa Aprili 14, 2023 na Katibu Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Taifa, Edna Lameck baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi tangu alipoteuliwa na Baraza Kuu la jumuiya hiyo.

"Mwenyekiti ataweka utaratibu mzuri kuhakikisha anakutana mara kwa mara na vijana mbalimbali kubadilishana mawazo na uzoefu kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili," amesema.

Mbali na hilo, amesema Aprili 17, mwaka huu jumuiya hiyo inatarajia kuanza ziara katika Mikoa sita, kutembelea mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT).

"Mwenyekiti atafanya ziara hii akiambatana nami kihakikisha umma inaelezwa na kuonyesha kile kinachofanywa na vijana wenzao ili nao wahamasike," amesema.

Edna aliteuliwa na Baraza Kuu kushika wadhifa huo, Machi 2023 akichukua nafasi ya Burugu Majenge aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo.

Mbali na Edna makabidhiano ya ofisi pia yamefanyika kwa nafasi ya Katibu wa Oganaizesheni, Mbarouk Mbarouk, aliyechukua wadhifa kutoka kwa Anzuruni Mtengwa.