Vanessa Mdee aunganishwa tuhuma dawa za kulevya

Mwanamuziki Vanessa Mdee maarufu, V-Money

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ametaja majina mengine ya watu sita wanaotakiwa kufika polisi kwa ajili ya kuhojiwa kwa tuhuma zinazowakabili.

Dar es Salaam. Msanii maarufu wa muziki nchini, Vanessa Mdee ametakiwa kufika kituo kikuu cha polisi cha Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za dawa za kulevya.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ametaja majina mengine ya watu sita wanaotakiwa kufika polisi kwa ajili ya kuhojiwa kwa tuhuma zinazowakabili.

Watu hao ni Tunda (msanii), Halidali Kavila, Amani, Kashozi na mfanya biashara Omary Sanga ambaye Makonda alisema amesababisha zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania huko kufungwa China na Hong Kong.