Vibanda vya wafanyabiashara Kirumba vyabomolewa

Vibanda vya wafanyabiashara Kirumba vyabomolewa

Muktasari:

  • Vibanda vya wafanyabiashara wadogo katika mtaa wa Kirumba kati vimebomolewa leo Alhamisi Julai Mosi, 2021 kwa amri ya baraza la ardhi na nyumba Mkoa wa Mwanza.

Mwanza. Vibanda vya wafanyabiashara wadogo katika mtaa wa Kirumba kati vimebomolewa leo Alhamisi Julai Mosi, 2021 kwa madai ya amri ya baraza la ardhi na nyumba Mkoa wa Mwanza.

Vibanda hivyo vinavyotazamana na soko la Rock City Mall vinabomolewa baada ya baraza hilo la ardhi kuwaamuru waondoe vibanda na vifaa vyao ndani ya siku kumi na nne kuanzia Juni 5, 2021.

Mfanyabiashara katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Japhet amesema waligoma kuondoka katika eneo hilo kwa sababu liko katika hifadhi ya barabara huku akidai hakuna sehemu ya barabara inayomilikiwa na mtu binafsi.

Dalali anayeendesha zoezi hilo, Shaaban Nassoro amesema anatekeleza maagizo aliyopewa na baraza hivyo hawezi kuzungumza zaidi.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi