VIDEO: Kauli ya kwanza ya Mo Dewji
Muktasari:
Bilionea nchini Tanzania, Mohamed Dewji 'Mo' amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kupatikana akiwa hai
Mo amepatikana alfajiri ya leo Jumamosi Oktoba 20, 2018
Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji 'Mo' anamshukuru Mungu kwa kunirejesha salama.
Mo aliyepatikana alfajiri ya leo Jumamosi Oktoba 20, 2018 amesema hayo kupitia akaunti ya Twitter ya Kampuni ya Mohamed Enterprise Limited (Metl Group).
"Namshukuru mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao."
"Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo jeshi la polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama," amesema Mo
Endelea kufuatilia Mwananchi