Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo wastaafu wajifungia kujadili mchakato wa Katiba mpya

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro

Muktasari:

  • Tayari Bunge limepitisha bajeti ya Sh9 bilioni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mchakato wa Katiba mpya. Hata hivyo, haijulikani ni mchakato huo utafikia tamati na nchi kupata Katiba mpya.

Dar es Salaam. Wizara ya Katiba na Sheria, imewakutanisha pamoja mawaziri wa sheria na wanasheria wakuu wastaafu na waliopo madarakani katika kikao chenye lengo la maoni yao kuhusu mchakato kupata Katiba mpya.

Waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika leo Agosti 28, 2023 jijini Dar es Salaam, ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman akiwa kama Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Wengine ni mawaziri wakuu wastaafu, John Malecela, Joseph Warioba na Mizengo Pinda. Pia, wapo mawaziri wa zamani wa Wizara ya Katiba na Sheria akiwemo Mary Nagu, Balozi Mathias Chikawe, Profesa Palamagamba Kabudi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk George Simbachawene ambaye pia ni Waziri wa Utumishi na Utawala Bora.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho, Dk Damas Ndumbaro amesema wameamua kukutana na viongozi hao ili kupata uzoefu wao kwa kuwa waliwahi kufanya kazi katika wizara hiyo, hivyo wana ufahamu na uelewa wa kutosha katika mchakato wa Katiba mpya.

"Tunaamini uzoefu mliokuwa nao katika wizara hii na katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba ambao ulikoma mwaka 2014, mna mengi ya kutushauri ili tuwe na mchakato mahsusi. Tunaamini tutajufunza mengi kutoka kwenu," amesema Dk Ndumbaro.

Waziri huyo amebainisha kwamba wizara yake imeamua kuliweka kama kipaumbele namba moja suala la elimu ya Katiba kwa wananchi kwa sababu tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania hawaifahamu Katiba, wengine hawajawahi hata kuiona.

Amesema ulichukulia umuhimu wa Katiba katika taifa lolote, wana wajibu wa kuhakikisha kwamba hiyo asiliamia 50 ya Watanzania wanaifahamu Katiba. Amesema wasipoifahamu, hatari ni kwamba wataamini hata upotoshaji unaofanya huko mitaani.

Kutokana na umuhimu huo, Wizara hiyo imekuja na Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Katiba kwa Umma (Mteku 2023/2026) ili kuhakikisha kwamba elimu ya Katiba inawafikia wananchi wote.

"Jambo hili tumelipa msukumo mahsusi tunaokwenda nao kwa miaka mitatu ili kuhakikisha kwamba Watanzania wote wanaijua Katiba yao," amesema Dk Ndumbaro.

Awali akizungumzia kikao hicho, Waziri mstaafu wa Sheria na Katiba, Dk Mary Nagu amesema endapo mabadiliko kwenye Katiba yatafanyika, basi yafanyike kikamilifu ili Katiba ya Tanzania ifanane na ya Marekani ilihodumu kwa miaka mingi huku ikifanyiwa marekebisho madogo madogo baada ya muda mrefu kupita.

"Mwaka 2026 tutakapoanza mchakato wa Katiba mpya, tuwe na unakika wa jambo ambalo litafanyika. Tuna nafasi ya kuangalia mambo gani tuyaweke, mambo gani yamepitwa na wakati tuyaondoe," amesema Dk Nagu.

Nyongeza na Brighton Samwel