Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana washauriwa kubadili mawazo

Muktasari:

Vijana wameshauriwa kuacha tabia ya kukimbilia mjini badala yake wajiunge na vyuo vya ufundi kutatua tatizo la ajira.

Iringa. Vijana wanaoishi vijiji vilivyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wameshauriwa kujiunga na vyuo vya ufundi stadi kupata ujuzi na kuondokana na tatizo la ajira na dhana ya kukimbilia mjini kutafuta.

Rai hiyo imetolewa na Makamu Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Rural Development Organization (RDO) la Mufindi, Obadia Ngailo wakati wa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo

Obadia amesema katika mafunzo ya ufundi stadi vijana wamefanikiwa kujiajiri na kuajiri wenzao kupitia mafunzo wanayopata huku lengo la shirika hilo likiwa ni kusaidia kuleta maendeleo vijijini kwa kutoa huduma kwa jamii kwa kuendelea hasa kwa Watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.

“Kutokana na ugumu wa ajira serikalini ni muhimu vijana kujifunza ufundi wa fani mbalimbali ili waweze kujiajiri na kujikomboa, hasa vijijini ili kufuta mawazo ya kukimbilia mjini kutafuta ajira”.

Amesema vijana wengi wa vijijini wanaamini katika kufanikiwa wakiwa mjini hivyo kupitia RDO tunatoa mafunzo ya ufundi stadi ili vijana wa vijijini waweze kupata elimu na kufanikiwa kiuchumi wakiwa katika vijiji vyao na kuviendeleza vijiji hivyo.

Kwa upande wake wanafunzi Joyce Sapoko,  mnufaika wa mradi wa RDO  amesema kuwa kupitia kozi walizosomea watakwenda kusaidia na kujiendeleza katika maeneo wanayoishi  kwa kufanya shughuli za ujasiriamali.

“Najisikia fahari kuingia katika chuo hiki na kweli kinatupatia elimu na pia elimu hii tunayoipata hapa itatusaidia kwa sababu tutakwenda hata kusaidia na kuwasaidia wenzetu maana tumetoka ngorongoro tutakwenda kufanya vizuri”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la RDO Fidelis Filipatali amesema kuwa shirika hilo lilianzishwa katika kijiji cha Mdabulo ikiwa lengo ni kuweka usawa wa vijijini na mjini huku ikisaidia kusomesha watoto kuanzia darasa la awali mpaka stashahada.

“Tuliamua kuweka kijijini shirika hili kwa sababu kuna wengine wanaona huduma nyingi zinakwenda mjini lakini tukaamua kuweka usawa ili kijiji kisitofautiane na mjini kwani hata kwasasa kuna watoto wengine wanatoka mjini lakini wanakuja kusoma huku kijijini kwa hiyo tumeamua kuweka usawa huo na watoto tunaowasaidia kupata elimu ni kuanzia awali hadi stashahada “alisema