Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijiji jirani Barrick Bulyanhulu vyanufaika miradi kufuga nyuki

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Wakazi wa Kijiji cha Buyange Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga wameanza kunufaika kupitia miradi ya kichumi ikiwemo ufugaji wa nyuki baada ya kupata mafunzo maalum nauwezeshaji kutoka mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu.

Shinyanga. Wakazi wa Kijiji cha Buyange Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga wameanza kunufaika kupitia miradi ya kichumi ikiwemo ufugaji wa nyuki baada ya kupata mafunzo maalum nauwezeshaji kutoka mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu.

Kupitia mradi huo wa ufugaji nyuki ambao ni moja ya miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) inayotekelezwa na mgodi huo, tayari baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamebadilisha hali zao kimaisha ikiwemo kujenga nyumba bora, kugharamia elimu kwa watoto wao na kuanzisha miradi mingine kuongeza kipato cha familia.

Belitha Nyawanga, mkazi wa kijiji cha Buyange ambaye ni miongoni mwa wanufaika wa mradi wa kufuga nyuki ameiambia Mwananchi kuwa kipato cha familia yake kimeongezeka tangu alipojiunga kwenye kikundi cha kufuga nyuki baada ya mafunzo kutoka kwa wataalam mwaka 2020.

‘’Tayari familia yangu imeanza ujenzi wa nyumba bora kutokana na mapato ya mradi wa kufuga nyuki," amesema Belita.

Mkazi mwingine wa Kijiji cha Buyange, Jeremia Nzima ameushukuru uongozi wa Barrick Bulyanhulu kwa kutekeleza mradi wa CSR unaogusa maisha ya wananchi moja kwa moja kupitia miradi ya kuongeza kipato huku akiiomba Serikali kupitia Halmashauri ya Msalala kuhakikisha wataalam wake wanatembelea vijijini kutoa ushauri kwa vikundi vya ujasiriamali.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Msalala, Judica Joel amesema halmashauri hiyo huendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu, lengo likiwa ni kuwawezesha kutumia vema fursa na mitaji yao.

"Kwa sasa tumeelekeza nguvu kutoa elimu kuviwezesha vikundi vya kufuga nyuki kuanza kusindika mazao ya nyuki,’’ amesema Judica

Agnes Andrew, mama lishe kutoka Kijiji cha Bunango ambacho ni miongoni mwa vijiji vya Kata ya Bugharama vinavyonufaika na miradi ya CSR anasema biashara yake imeimarika kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa manunuzi wa wananchi.

Katibu wa kikundi cha Wikondele ambacho ni miongoni mwa vikundi vinavyonufaika na miradi ya CSR kutoka Barrick Bulyanhulu, Daniel Samson amesema mradi wa kufuga nyuki umewawezesha wana kikundi kukopeshana mitaji ya kuanzisha miradi mingine ya ujasiriamali.

Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo amesema pamoja na elimu ya kufuga nyuki, wanachama wa vikundi vya kufuga nyuki pia hupata fursa ya ziara za mafunzo ikiwemo kuhudhuria maonyesho ya maeneo tofauti kujifunza mbinu za kuongeza tija katika ufugaji wa nyuki.