Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi wa dini watakiwa kukemea ukatili wa kijinsia

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Bashiru Muhoja  (aliyesimama) akizungumza na wachungaji na wanandoa wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Muktasari:

Viongozi wa dini wametakiwa kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa waumini ili kuondokana na matendo ya ukatili katika familia zao na jamii.

Iringa. Viongozi wa dini wametakiwa kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa waumini ili kuondokana na matendo ya ukatili katika familia zao na jamii.

Wilto huo umetolewa na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Kihesa, Gaitan Mkemwa wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la World Vision.

Mchungaji Gaitan amesema kupitia siku 16 za kupinga ukatili, viongozi wa dini wasimame na kueleza kama Mungu alivyokusudia na kama jamii inavyotaka ifike mahali watoe malezi na mafundisho sahihi yanayoonyesha kuheshimiana kwa wanadamu.

"Mwanaume amuheshimu mwanamke na mwanamke amuheshimu mwanaume hivyo elimu katika dini zetu na madhehebu tuliyonayo iwe ni sehemu ya kutoa maelezo ya kukataa, kukemea na kupinga ukatili na maombi yafanyike ili kukomesha ukatili wa kijinsia katika dunia hii"amesema na kuongeza

“Kutokutoa huduma ya kiroho au kutii agizo la Mungu ndio maana shetani anajiinua na kuona kwamba hata tukizungumza jambo la ukatili halifikii mahali kwa sababu viongozi wa dini hatupo sawa sawa na makusudi ya Mungu, viongozi wa dini wamefika mahali wanataka kuingia kufanya kazi badala ya kutoa huduma ya kiroho"amesema

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa, Bashiru Muhoja amewataka wazazi na walezi mkoani huko kuwalinda watoto wao dhidi ya ukatili wa kijinsia.

“Wengi wa matukio haya hufanywa na wanandugu na familia kuamua kutokutoa taarifa katika vyombo vya sheria kwa maana ya kulindana na kuogopa kuipa aibu familia zao hivyo nawaomba tuachane na dhana hii tutoe taarifa ili watuhumiwa wawajibishwe kwa mujibu wa sheria” amesema Muhoja na kuongeza

“Kuna familia zingine ukatili huo hufanywa na baba kwa watoto na mama hufumbia macho kwa kulinda ndoa yake na kufanya familia nzima kuteseka na ndoa hiyo kukosa amani”

“Jamii inatakiwa isifanye matukio ya ukatili,na iwapo itatokea jamii itoe taarifa sehemu husika ili htua za kisheria zichukuliwe ili kukomesha matukio haya” amesema

Mratibu wa jinsia na ushawishi wa Shirika la World Vision Tanzania, Geofrey Kisemba amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuwa na jamii iliyo salama ambayo haifanyiwi ukatili wa kijinsia na kuwa na watoto salama ambao hawafanyiwi ukatili wa kijinsia.

Kisemba amesema kuwa ukatili wa kijinsia hauleti usitawi kwa watoto iwe ni katika afya elimu uchumi hayawezi kuwa mazuri endapo jamii itakuwa inafanya ukatili wa kijinsia iwe kwa wanaume au kwa wanawake.

“Maendeleo katika jamii hayawezi kupatikana kama ukatili wa kijinsia utaendelea katika familia, jamii ijikite katika kupinga ukatili wa kijinsia katika familia na kuepuka mila na destuli ambazo ndio chanzo kikubwa cha ukatili”amesema Kisemba na kuongeza

"Suala la la kiuchumi ni la msingi sisi kama wadau na Serikali na mashirika mengine ya kimataifa ni lazima tutimize wajibu wetu kwa kuhakikisha tunawatoa hawa wananchi kwenye dimbwi la umasikini ili wasiwaozeshe watoto wao wakiwa wadogo na wasiweze kuwafanya watoto wao wadogo wapate mimba wakiwa na umri mdogo kwa sababu umasikini ukiwa mkubwa na ukatili unakuwa mkubwa"

Kisemba amesema kuwa wamewashirikisha wanandoa katika uzinduzi huo wa siku 16 kwa sababu wanaamini kuwa ili jamii iwe salama ni lazima familia iwe salama kwa kuwa wanandoa ndio kiini cha jamii salama.

"Wanandoa wakiwa na maelewano ndani ya nyumba tunaamini watawahudumia watoto na watakuwa salama,lakini endapo wanandoa wakipigana na kutokuelewana tunaamini hata watoto watapata shida na kujikuta wanafanyiwa utalii".