Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vituo 490 kutumika uchaguzi Mbarali

Muktasari:

  • Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Mbarali, Missana Kwangura amesema mpaka sasa vyama 13 vimesimamisha wagombea ambavyo pia vilishiriki  kampeni kwa siku 30 kuwanadi wagombea 13 kati ya hao  watano ni wanawake.

Mbeya. Vituo 490 vinatarajia kutumika kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa nafasi ya ubunge  Jimbo la Mbarali, Mkoa wa Mbeya, ambalo lilikuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge Francis Mtega kufariki dunia kwa ajali ya treka dogo aina ya Power Tillar.

 Akizungumza na waandishi wa habari Leo Jumatatu Septemba 18, 2023 msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mbarali na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Missana Kwangaru amesema mpaka sasa vyama 13 kati ya 14 vitashiriki kugombea nafasi hiyo.

“Kulikuwa na vyama 14 ambavyo wagombea wake walichukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge lakini Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mgombea wake alijitoa na akurejesha fomu,”amesema.

Ametaja majina ya vyama na wagombea kwenye mabano kuwa ni Halima Abdallah (AAFP), Kirufi Modestus (ACT -Wazalendo), Hussein Hassan (ADA), Abdallah Hashim (ADC) Mwataka Exsavery (CCK), Bahati Ndingo (CCM).

Wengine ni Barick Mwanyalu (Demokrasia Makini), Osward Mdeva (DP), Fatuma Rashid (NLD), Morris Thomas (TLP), Mwajuma Milambo (UMD), Seleleka Laurent (UDP) na Mery Daud (UPDP). 

Kwangura amesema kuwa tayari maandalizi yako vizuri na wapo viongozi mbalimbali wakiwepo waliotoka  Tume ya Taifa ya Uchaguzi akiwepo Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Tehama na kwamba kutakuwa na mfumo rasmi wa kuhesabiwa kura wa CMS ambao utarahisisha zoezi hilo.

“Tayari tulitoa elimu kwa wagombea na viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha suala la maadili linapewa kipaumbele ili kuondoa manung'uniko sambamba na matokeo kutangazwa kwa wakati ili kila wagombea watakaoshiriki kuridhika na matokeo ya kura zitakazopigwa,” amesema.

Amesema kuwa Mawakala wamepewa maelekezo kuhakikisha wanapewa fomu namba 21 (b) sambamba na kusimamia zoezi hilo kwa umakini mkubwa ili kuepuka manung'uniko kwa washiriki wanaowania nafasi ya ubunge jimbo la Mbarali katika uchaguzi mdogo unaofanyika kesho Septemba 18 mwaka huu.