Vodacom yazindua teknolojia ya 5G, Serikali yajivunia mafanikio

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hilda Bujiku akizungumza akati wa huduma ya mpya teknolojia ya 5G

Muktasari:

Vodacom yazindua teknolojia mpya ya 5G itakayoleta mapinduzi katika mageuzi ya sekta ya viwandal, huku Serikali ikibainisha kuwa Tanzania imekuwa ya kwanza miongozi wa nchi za Afrika zilizoingia katika programu hiyo.

Dar es Salaam. Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC imezindua huduma ya mpya teknolojia 5G ikisema italeta mapinduzi na kuongeza ushiriki wa Taifa katika kuleta mageuzi ya nne ya viwanda.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Septemba Mosi, 2022 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hilda Bujiku wakati wa halfa ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.

"Teknolojia hii ya 5G inakuja na fursa kubwa hapa nchini kwa wabunifu kuleta bidhaa na huduma mpya kwa wananchi. Vodacom sio tu itaendelea kubuni huduma mpya bali kuwezesha jamii ili kutimiza ndoto za kujenga Taifa bora.

Katika uzinduzi huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliyeeleza kuwa, Mei mwaka huu aliahidi Bungeni kwamba Tanzania itaanzisha 5G hapa nchini jambo hilo limetia leo kwa kampuni ya Vodacom kulitekeleza.

"Tuliposema ilikuwa kama ndoto lakini leo karibu miezi mitatu, lakini Vodacom wametekeleza na kutusaidia kuingia kwenye orodha ya nchi chache Afrika zilizoanzisha huduma ya teknolojia ya 5G.Vodacom wamekuwa wa kwanza kwenye mambo mengi wameanza na M-Pesa na mambo mengine nawashukuru," amesema Nape.