Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waandishi wa habari wazuiwa uchaguzi CCM Kagera

Muktasari:

  • Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimealika baadhi ya waandishi wa mkoa wa Kagera kushiriki katika uchaguzi wa chama hicho mkoa wa Kagera huku wengine wakizuiliwa mlangoni kwa kile kilichoelezwa ni kutokualikwa.

Bukoba. Baadhi ya waandishi wa habari wamezuiliwa kuingia kwenye ukumbi wa uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kagera huku ikielezwa kuna waandishi wamealikwa kwa ajili ya kuandika habari katika uchaguzi huo.

Mmoja wa watu waliokuwa mlangoni akiruhusu wajumbe kuingia ukumbini katika uchaguzi huo unaofanyika leo Jumanne, Novemba 22, 2022 amekuja na majina ya vyombo vitano akisema waandishi wake wanaruhusiwa kuingia ukumbini huku wengine wakizuiliwakuingia.

Katibu wa CCM mkoa wa Kagera, Christopher Palangyo alipofuatwa na waandishi hao alidai wasubiri watapata utaratibu badaye na hadi wagombea wanajinadi waandishi hao walikuwa nje ya ukumbi.

Wagombea nafasi ya uenyekiti CCM Mkoa wa Kagera ni Novatus Nkwama, Medard Mshobozi, Nazir Kalamagi na Kostansia Buhiye  na msimamizi wa uchaguzi huo ni Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Akson.