Wabunge Ulaya wataka maelezo 'kashfa ya sofa'

Thursday April 08 2021

Brussels, Ubelgiji (AFP). Wabunge wa Umoja wa Ulaya leo Alhamisi wametaka maelezxo kutoka kwa waofisa wawili wa juu kuhusu kashfa ya kidiplomasia baada ya kiongozi wa Kamisheni, Ursula von der Leyen kutopatiwa kiti wakati wa mazungumzo na rais wa Uturuki.

Tukio hilo, lililopachikwa jina la "kashfa ya sofa", imeibua tuhuma dhidi ya vitendo vya Uturuki dhidi ya wanawake na Umoja wa Ulaya, jinsia jijini Brussels, na mzozo wa ndani baina ya taasisi za umoja huo.

Suala hilo limejikita katika dakika zisizo za kawaida mwanzoni mwa mazungumzo kati ya von der Leyen, rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel na kiongozi wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan jijini Ankara JUmanne.

Wakati viongozi wawili wanaume walichukua viti viwili, von der Leyen, ambaye ni kipofu, alibaki amesimama kabla ya kuongozwa kwenda kukaa katika sofa lililokuwa karibu.

"Uhusiano wa EU-Uturuki ni muhimu. Lakini umoja wa EU na kuheshimu haki za binadamu, zikiwemo za wanawake, ni muhimu pia," aliandika mbunge kutoka Hispania, Iratxe Garcia Perez, ambaye ni kiongozi wa wanaharakati wa Kisoshalisti na Kidemokrasia bungeni, katika akaunti yake ya Twitter.

Alisema aliomba mazungumzo na Von der Leyen na Michel "ili kufafanua kilichotokea na ni jinsi gani ya kuheshimu taasisi za Umoja wa Ulaya".

Advertisement

Ombi hilo lilifanana na la kiongozi wa chama cha kihafidhina cha Watu wa Ulaya ktika Bunge la EU, Manfred Weber, ambaye aliiambia Politico kuwa safari ya kwenda Ankara imegeuka kuwa alama ya kutokuwepo kwa umoja baina ya viongozi wa juu wa Ulaya.

Mkutano huo na Erdogan ulikuja katika kipindi nyeti kutokana na umoja huo na Uturuki kuwa katika mikakati ya kujenga upya uhusiano baada ya kuathiriwa na wasiwasi baina ya pande hizo mbili mwaka jana.

Advertisement