Wabunge wateule watua bungeni kula kiapo

Dk Bashiru, Mulamula wasubiri kuapishwa bungeni kiapo

Muktasari:

  • Wabunge watatu walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jana Machi 31, 2021 wamewasili bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 kwa ajili ya kuapishwa na kuanza majukumu yao mapya.

Dodoma. Wabunge watatu walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jana Machi 31, 2021 wamewasili bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 kwa ajili ya kuapishwa na kuanza majukumu yao mapya.

Mwananchi Digital limewaona wabunge hao wakiwa katika viwanja vya Bunge wakisubiri kula kuanza kwa kikao cha tatu ili waapishwe.

Wabunge hao ni Dk Bashiru Ally ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa katibu mkuu kiongozi, Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

Wabunge wateule watua bungeni kula kiapo

Dk Bashiru aliwasili ukumbini saa 2:05 asubuhi na kutoka kisha akarejea tena saa 2:13.

Mapema aliposhuka kwenye gari alipokewa na askari wa BungeĀ  aliyemuongoza kuingia katika ukumbi huo na kusubiri maelekezo mengine.

Balozi Mulamula aliwasili bungeni akiwa amevaa barakoa na alisindikizwa na mmoja wa maofisa wa Bunge huku akifuatwa nyuma na Balozi Mbarouk.