Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachumi waichambua ‘mikopo ya mitaani’

Muktasari:

  • Mchambuzi wa Masuala ya Uchumi, Oscar Mkunde ameshiriki mjadala wa TwitterSpace ya Mwananchi yenye mada ‘ongezeko la taasisi za mikopo nchini, ni fursa au changamoto kwa jamii?’ na kueleza faida na hasara za mikopo hiyo. 

Dar es Salaam. Mchambuzi wa Masuala ya Uchumi, Oscar Mkunde amesema, wanaotoa mikopo hii ni wafanyabiashara, kuna mwaka jarida la uchumi limeandika katika kampuni zilizotengeneza faida kubwa ni kampuni hizi za kukopesha na sio kusaidia watu.

Mkude amesema hayo wakati akichangia mada ya TwitterSpace ya Mwananchi yenye mada ‘ongezeko la taasisi za mikopo nchini, ni fursa au changamoto kwa jamii?’ leo Jumatano, Julai 12, 2023.

“Mikopo hii ilianzishwa kusaidia wakopaji wadogo, benki zinasaidia wakopaji wakubwa, hii mikopo midogomidogo inaangalia watu wa chini,” amesema

Amesema kuna watu wanaokopa kwenda kula, jitahidi ukope ukafanye biashara ukianza kula mkopo wenyewe ni sawa na kula mbegu na hutoweza kurudisha.

“Mikopo hii inafeli kwasabaabu tunakopa na kwenda kula, pia mikopo inayokopwa ni kwa ajili ya mapenzi na wakopaji wengi sio wajasiriamali.”

Amesema taasisi hizi hawaulizi namna utakayorejesha una cherehani au una kitu chochote unakopeshwa mkopo, hii ni tofauti na ukienda benki utaulizwa unafanya biashara gani au kazi gani.

“Mikopo hii inajenga picha ya unyonyaji kwanini wameangalia faida sana na hawazingatii tena miongozo ya zamani kwamba unafanya biashara gani au kukupa elimu,” amesema

Kwa upande wake, Mchambuzi wa Masuala ya Uchumi na Mtaalamu wa Benki, Cleopa Lema amesema watumishi wengi wa umma wanatakiwa kupewa elimu ya kisaikolojia kwani asilimia kubwa wapo kwenye mikopo hii tunayoita umiza.

“Katika watumishi wa umma 100 watumishi 20 wanaacha kadi zao kwenye hizo taasisi baada ya kukopa, hii ni kwasababu wameshakopa benki na sasa hawakopesheki,” amesema

Amesema, “mtu anaweza kuambiwa unakopeshwa Sh1 milioni riba asilimia tano haulizi hiyo riba ni kwa muda gani, akianza kukatwa unalalamika mbona makato hayaishi.”

Lema amesema asilimia kubwa ya Watanzania, “uelewa wetu kwenye mikopo ya biashara ni kwenye vitu vichache sana, lakini kwa watumishi kwasababu anajua atakatwa kwenye mshahara hajui hatari atakayopitia.”