Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara Kariakoo washauriwa kuchukua bima

Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Kaimu Abdi Mkeyenge  (Kulia) akiwa katika makubaliano ya utoaji huduma za bima kwenye soko la Kariakoo. Kushoto ni, Ashraph Abdulkarim ambae ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.

Muktasari:

  • Uwepo wa bima huongeza uaminifu kwa taasisi za kifedha na hurahisisha upatikanaji wa mikopo, jambo linalosaidia kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo wameshauriwa kukata bima za biashara zao ili kujilinda dhidi ya majanga mbalimbali yakiwemo moto, mafuriko na majanga mengine yanayoweza kusababisha hasara kubwa.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Ashraph Abdulkarim, jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya shirika hilo na Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Amesema soko hilo limewahi kuathirika vibaya na janga la moto lililosababisha hasara kubwa kwa serikali, hivyo ni muhimu maboresho yaliyofanyika kulindwa kupitia huduma ya bima.

Meneja wa Mipango na Biashara wa Shirika hilo, Mwinga Luhoyo, amesema soko kwa sasa lina zaidi ya maeneo 1,900 ya biashara na linatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 4,000 kwa Watanzania, hivyo kuna umuhimu wa kulinda uwekezaji huo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Kaimu Abdi Mkeyenge, amesema shirika hilo limejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa Kariakoo na wananchi kwa ujumla kuhusu umuhimu wa bima, sambamba na kutoa huduma kwa gharama nafuu ili kulinda mali za serikali, wananchi na taasisi binafsi.


Amesema bima ni njia bora ya kuhakikisha biashara zinaendelea hata baada ya janga kutokea, kwani humuwezesha mfanyabiashara kupata fidia na kuanza upya bila kuathiri uzalishaji au ajira. Ameongeza kuwa uwepo wa bima huongeza uaminifu kwa taasisi za kifedha na hurahisisha upatikanaji wa mikopo, jambo linalosaidia kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Mkeyenge amesisitiza kuwa kwa mazingira ya sasa ambapo majanga yanatokea bila kutarajiwa, ni muhimu kwa wafanyabiashara kujenga utamaduni wa kutumia bima kama sehemu ya mkakati wa kulinda rasilimali zao na kuchochea ustawi wa kiuchumi wa taifa.