Wafanyabiashara Maswa walilia elimu ya tozo
Baadhi ya wafanyabiashara wilayani Maswa wakiwa katika mafunzo ya mabadiliko ya Sheria ya Kodi ya Mwaka 2022. Picha na Samirah Yusuph
Muktasari:
- Baadhi ya wafanyabiashara wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu waimeiomba Mamlaka ya Mapato (TRA) kutumia lugha za kiungwana zinazoshawiahi wananchi kulipa Kodi.
Maswa. Baadhi ya Wafanyabiashara wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu waimeiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutumia lugha za kiungwana zinazoshawiahi wananchi kulipa Kodi.
Wakiwa katika mafunzo na maofisa wa TRA yenye lengo la kujenga uelewa wa mabadiliko ya kodi kulingana na Sheria ya Fedha ya mwaka 2022 leo Septemba 19, wamesema licha ya kuwa ulipaji wa kodi upo kisheria, maofisa wa mamlaka hiyo wanapaswa kuwa na kauli zenye ushawishi.
“Hakuna haja ya kuwapa wateja vitisho na mlolongo mrefu wa maelezo yanayokatisha tamaa kwa walipa kodi na kusababisha maisha ya kukwepana na kukimbizana.
“TRA ijenge mahusiano mzuri na wafanyabiashara ili kila Mtanzania awiwe na kuona anawajibu wa kutoa kodi ili kuchangia maendeleo," amesema James Nila mfanyabiashara wilayani Maswa.
Kwa upande wake Meneja TRA Mkoa wa Simiyu, Naye Mtandika amesema pamoja na mabadiliko ya sheria, wanajukumu la kuwakumbusha wajibu wa msingi wa kulipa kodi kwa hiari bila kufukuzana wala kukimbizana.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa wazalendo kwa kulipa kodi ya serikali kwa maendeleo ya Taifa.
“Serikali haifanyi biashara, inakusaya kodi kwa ajili ya kazi za maendeleo, sasa jambo kubwa kwa wananchi ni kulipa kodi na serikali inarudisha kodi hizo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 Wilaya ya Maswa ilikusanya Sh717 milioni sawa asilimia 92 ya lengo la ukusanyaji wa mapato ambapo mwaka huu 2012/2023 lengo llililowekwa ni Sh 940.3 milioni.