Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara wametakiwa kukata bima za majanga ya moto

Kaimu Meneja wa kampuni ya Bima ya BUMACO, Gasto Mrema akitoa elimu juu ya majanga. Picha na Fina Lyimo

Muktasari:

Wafanyabiashara nchini wametakiwa kukata bima za majanga ya moto ili kuondokana na hasara zinazotokana na kuungua kwa biashara pamoja na majengo.

Moshi. Wafanyabiashara nchini wametakiwa kukata bima za majanga ya moto ili kuondokana na hasara zinazotokana na kuungua kwa biashara pamoja na majengo.

Haya yamesemwa leo Februari 26, 2022 na Meneja Msaidizi wa kampuni ya bima BUMACO, Gasto Mrema kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kilimo gulio yaliofanyika katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema hivi karibuni kumekuwepo na majanga ya kuungua na kuteketea moto bidhaa za wafanyabiashara masokoni na hatimaye wafanyabiashara kushindwa kuendeleza biashara kwa kukosa mitaji

Amesema ni vyema wafanyabiashara wakajiunga na bima za majanga ili waweze kupata mitaji pindi mali zoa zinapopata majanga ya moto.


"Nashauri wafanyabiashara na wananchi wa kawaida wakate bima za majanga ili waweze kupata fidia pindi mali zao zinapoteketea kwa moto"amesema

Meneja huyo amesema BUMACO imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi hususani katika bima za majanga ya moto, sehemu za biashara masokoni, mashuleni na majengo ya nyumba, na kwamba mwitikio ni mdogo wa ukataji bima.

"Kwa nchi nzima tangu tuanze huduma ya ukataji bima ya majanga tuna wanachama milioni moja lengo ni kupata wanachama milioni mbili kwa mwaka"amesema Mrema

Mmoja wa wajasiriamali, Neema mwendo amesema bado wananchi hawana uelewa kuhusiana na bima za majanga hivyo elimu zaidi inahitajika kwa jamii.

Amesema endapo wananchi watapata elimu ya bima ya majanga itawasaidia kupunguza machungu ya kuunguliwa na biashara zao kwa kulipwa bima pindi majanga yanapotokea.