Wafanyakazi Benki Ya Exim Washiriki NMB Marathon kusaidia Matibabu Ya Fistula Kwa Kina Mama

Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakijipongeza na medali zao baada ya kushiriki mbio za Hisani za NMB Marathon zilizokuwa na kauli mbiu 'Mwendo wa Upendo,' zikilenga kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 1 ili kufanikisha mpango wa matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo mapema hii leo. Mbali na kushiriki mbio hizo Benki hiyo pia ilitoa mchango wa fedha kiasi cha Sh Mil 10 kwa waandaaji wa mbio hizo  ili kuunga mkono jitihada hizo

Dar es Salaam. Katika kuunga mkono agenda ya kusaidia matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo, wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wameungana na maelfu ya Watanzania wengine akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kushiriki mbio za Hisani za NMB Marathon zilizokuwa zikilenga kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia matibabu hayo.

Tupo tayari kwa mbio! Ndivyo wanavyoonekana wakisema wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania walipojitokeza kushiriki mbio za Hisani za NMB Marathon zilizokuwa na kauli mbiu 'Mwendo wa Upendo,' zikilenga kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 1 ili kufanikisha mpango wa matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo mapema hii leo. Mbali na kushiriki mbio hizo Benki hiyo pia ilitoa mchango wa fedha kiasi cha Sh Mil 10 kwa waandaaji wa mbio hizo  ili kuunga mkono jitihada hizo

Mbio hizo ambazo zimefanyika leo Jumamosi Septemba 25, 2021 jijini Dar es Salaam zikiwa na kauli mbiu 'Mwendo wa Upendo,' zililenga kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 1 ili kufanikisha mpango huo.

Mbali na kushiriki mbio hizo Benki hiyo pia ilitoa mchango wa fedha kiasi cha Sh10 milioni kwa waandaaji wa mbio hizo ili kuunga mkono jitihada hizo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakishiriki mbio hizo.

Baada ya kushiriki mbio hizo wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania walijipongeza kwa kupata medali.