Wafanyakazi TPA kizimbani wakituhumiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh694 milioni

Dar es Salaam. Wafanyakazi wanne wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kitengo cha uhasibu na mmoja aliyekuwa kibarua wa mamlaka hiyo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la kuingiza data za uongo kwenye mfumo malipo na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh694.07 milioni